News

Announcements, match reports and updates from the Tanzania Premier League Board.

NTIBAZONKIZA MTAALAMU WA PENATI LIGI KUU YA NBC.

Jumla ya mabao 35 ya penati yamefungwa kwenye Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2023/2024 huku Said Ntibazonkiza akiibuka kinara kwa kufunga mabao Mengi (7). Ntibazonkiza alifunga mabao hayo kwenye michezo dhidi ya Prisons, Kagera Sugar, KMC, Mashujaa, Singida FG, Geita Gold na JKT Tanzania. Stephane Ki Aziz wa Young Africans anafuatia akifunga mabao matatu,…

Yahaya Abushehe · Read more

JKT YASALIA LIGI KUU YA NBC, TABORA KUIVAA BIASHARA UNITED.

JKT Tanzania imefanikiwa kubakia Ligi Kuu ya NBC baada ya hii Leo kutoka suluhu na Tabora United kwenye mchezo wa pili wa mtoano hivyo JKT Tanzania kusonga mbele kwa jumla ya mabao 4-0. Mchezo wa kwanza wa mtoano uliochezwa kwenye uwanja wa Ali hassan Mwinyi mkoani Tabora ulishuhudia wenyeji Tabora United wakikubali kichapo cha…

Yahaya Abushehe · Read more

GEITA GOLD YAUNGANA NA MTIBWA NBC CHAMPIONSHIP.

BAADA ya pazia la Ligi Kuu ya NBC Msimu wa 2023/2024 kumalizika rasmi jana Mei 28 na kushuhudia Geita Gold ikiungana na Mtibwa Sugar kushuka daraja na mwakani kushiriki Ligi ya NBC Championship. Geita Gold ilikusanya alama 25 kwenye michezo 30 ikishinda michezo mitano ikifungwa 15 na kupata sare michezo 10 ambapo alama hızo…

Yahaya Abushehe · Read more

LIGI KUU YA NBC KUHITIMISHWA LEO.

Ligi Kuu ya NBC inafika tamati Leo Mei 28 kwa michezo nane ikihusisha timu zote 16 Zinazoshiriki Ligi Kuu ya NBC kupigwa kuanzia saa 10:00 alasiri kwenye mikoa saba tofauti. Michezo ya leo itaamua hatma ya baadhi ya timu ikiwemo vita ya nafasi ya pili, nani kushuka daraja, nani kucheza mtoano (Playoff) na vita…

Yahaya Abushehe · Read more

MTIBWA SUGAR YASHUKA DARAJA.

LIGI Kuu ya NBC imeendelea kwa michezo nane inayohusisha timu zote 16 zinazoshiriki Ligi Kuu ya NBC kuchezwa kuanzia saa 10:00 alasiri kwenye mikoa Saba tofauti. Baada ya kichapo cha mabao 3-2 kutoka kwa Mashujaa, Rasmi Mtibwa Sugar imeshuka Daraja na itashiriki Ligi ya NBC Championship msimu ujao wa 2024/2025. Ligi Kuu ya NBC…

Yahaya Abushehe · Read more

BIASHARA YAIANZA VEMA VITA YA KUPANDA LIGI KUU YA NBC.

MCHEZO wa kwanza wa mchujo wa timu za NBC Championship kupanda Ligi Kuu ya NBC Kati ya BIashara United na Mbeya kwanza umemalizika kwa Biashara United kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mbeya kwanza. Mabao ya Biashara United yamefungwa na Abeid Othman dakika ya 22 na Boban Bogere dakika ya 34 na…

Yahaya Abushehe · Read more

YANGA BINGWA LIGI KUU YA NBC.

USHINDI wa mabao 3-1 dhidi ya Mtibwa Sugar umeipa timu ya Yanga ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2023/2024 baada ya kufikisha jumla ya alama 71 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yeyote . Huu ni ubingwa wa tatu mfululizo wa Ligi Kuu ya NBC kwa Young Africans tangu msimu wa 2021/2022 hadi…

Yahaya Abushehe · Read more

AFRICAN SPORTS BINGWA FIRST LEAGUE 2023/24.

TIMU ya African Sports ya Tanga imefanikiwa kuwa bingwa wa Ligi ya First League msimu wa 2023/24 baada ya kuifunga Kiluvya ya Dar es Salaam bao 1-0. African Sports imefanikiwa kutwaa ubingwa huo bila kupoteza mchezo wowote katika mashindano ya First League Nane Bora yaliyofanyika Tanga kwenye uwanja wa Mkwakwani. African Sports imefanikiwa kupanda daraja…

Honest Mwanitega · Read more

KILUVYA, AFRICAN SPORTS ZATINGA FAINALI YA FIRST LEAGUE NANE BORA.

TIMU za Kiluvya ya Dar es Salaam na African Sports ya Tanga zimefanikiwa kutinga fainali ya mashindano ya First League Nane Bora baada ya kushinda michezo yao ya nusu fainali. Kiluvya iliyocheza dhidi ya Malimao ya Dar es Salaam imeshinda kwa mikwaju ya penati 4-2 baada ya kutoka suluhu katika dakika 120. African Sports ilishinda…

Honest Mwanitega · Read more