News

Announcements, match reports and updates from the Tanzania Premier League Board.

KMC WAVUNJA MWIKO KWA SIMBA

Baada ya kusubiri kwa takribani misimu minne ya Ligi kuu bila kupata alama yoyote mbele ya Simba, KMC wamevunja mwiko huo baada ya kupata sare ya mabao mawili jana Septemba 7, 2022 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa. Kabla ya mchezo wa jana, KMC tangu walipopanda daraja msimu wa 2018/2019 walicheza jumla ya michezo nane ya…

Honest Mwanitega · Read more

RAUNDI YA TATU IKIENDELEA, KWA MKAPA MOTO KUWAKA TENA LEO

Raundi ya tatu ya Ligi Kuu ya NBC inaendelea tena leo kwa michezo miwili, Mtibwa Sugar watawakabili Ihefu SC kwenye uwanja wa Manungu, Morogoro saa 10:00 Alasiri huku saa 1:00 usiku Simba SC wakicheza na KMC FC kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa. Wakizungumza na waandishi wa habari makocha wa Simba na KMC wamesema hali ya…

Honest Mwanitega · Read more

HAPATOSHI KWA MKAPA LEO

Dar es Saalam na viunga vyake itasimama kwa dakika 90 kupisha mchezo wa kwanza wa ‘derby’ ndani ya msimu huu wa 2022/2023 ukizikutanisha Yanga SC na Azam FC katika uwanja wa Benjamin Mkapa leo Septemba 6, 2022 saa 1:00 usiku. Mara ya mwisho timu hizi zilikutana Aprili 6, 2022 katika uwanja wa Azam Complex Chamazi…

Honest Mwanitega · Read more

WANAHABARI WATAKAOHUDHURIA SEMINA YA KUWAJENGEA UWEZO

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imeandaa Semina ya siku moja ya kuwajengea uwezo Wanahabari wanaoandika habari za michezo (hasa mpira wa miguu). Semina hiyo itafanyika kuanzia saa 2:00 asubuhi Jumatatu Agosti 29, 2022 kwenye ukumbi wa mikutano uliopo ghorofa ya kwanza, Jengo la NSSF (Mafao House) lililopo Ilala Boma mkoani Dar es Salaam. Ifuatayo…

James Onesmo · Read more

LIGI KUU YA NBC MWENDO MDUNDO

Ligi Kuu ya NBC raundi ya pili imetamatika jana Agosti 21, 2022 kwa michezo minne kuchezwa na kukamilisha jumla ya michezo minane katika raundi ya pili. Mchezo wa mapema ulizikutanisha Mtibwa Sugar na Ruvu Shooting saa 8:00 mchana katika uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro na Mtibwa Sugar kushinda kwa mabao 2-1. Michezo miwili ya…

James Onesmo · Read more

MZUNGUKO WA PILI LIGI KUU YA NBC

Ligi Kuu ya NBC inaendelea hii leo kwa mchezo mmoja kuchezwa baina ya Ihefu SC na Namungo FC katika uwanja wa Uhuru kuanzia saa 10:00 alasiri. Ihefu wanatumia uwanja wa Uhuru kama uwanja wao wa nyumbani baada ya uwanja wao wa Highland Estates kufungiwa kutokana na kutokidhi vigezo vya kikanuni na sheria za mpira wa…

James Onesmo · Read more

KIVUMBI CHA LIGI KUU YA NBC KUANZA LEO

Pazia la Ligi kuu ya NBC msimu wa 2022/2023 linafunguliwa rasmi hii leo Agosti 15, 2022 kwa timu nne za Ihefu SC, Ruvu Shooting FC, Namungo FC na Mtibwa Sugar FC kushuka katika viwanja viwili kuzisaka alama tatu. Mchezo wa kwanza wa ufunguzi utazikutanisha Ihefu dhidi ya Ruvu Shooting majira ya saa 10:00 alasiri katika…

James Onesmo · Read more

KLABU LIGI KUU ZINAVYOVUNA KUTOKA SEMINA YA UEFA

SEMINA ya Maendeleo ya Ligi inayoendeshwa na UEFA chini ya mradi wao wa UEFA Assist imeingia siku ya nne leo kwenye Hotel ya Golden Tulip iliyopo Dar es Salaam. Leo washiriki wa semina hiyo inayotarajiwa kukamilika Januari 15, 2022, wamepata nafasi ya kujifunza masuala mbalimbali zikiwemo mbinu za kuziongezea kipato klabu zao. Semina hiyo inashirikisha…

Karim Boimanda · Read more