News

Announcements, match reports and updates from the Tanzania Premier League Board.

MBIO ZA UFUNGAJI BORA ZAPAMBA MOTO LIGI KUU YA NBC.

MZUNGUKO wa 16 umekamilika kwa timu zote za Ligi Kuu ya NBC huku vita ya kuwania ufungaji bora ikizidi kushika kasi na Elvis Rupia akiendelea kushikilia usukani wa kinyang’anyiro hicho. Rupia anaongoza baada ya kupachika mabao nane hadi sasa na kuisaidia timu yake kufikisha alama 30 na kukaa nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi…

Honest Mwanitega · Read more

MZUNGUKO WA 17 NBC CHAMPIONSHIP KUKAMILIKA LEO.

MZUNGUKO wa 17 wa Ligi ya Championship ya NBC unatamatika leo kwa mchezo kati ya Transit Camp ya Dar es salaam na Stand United ya Shinyanga saa 10:00 alasiri katika uwanja wa Mabatini Mkoani Pwani. Transit Camp ipo nafasi ya 13 kwenye msimamo wa Ligi ya Championship ya NBC ikiwa na alama 10 sawa na…

Yahaya Abushehe · Read more

SIMBA WAENDELEZA UBABE DHIDI YA TABORA UNITED

Ligi Kuu ya NBC ambayo ni Ligi ya nne kwa ubora barani Afrika imeendelea kwa mchezo mmoja uliochezwa mkoani Tabora ambapo timu ya Tabora United waliwakaribisha Simba katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi. Mchezo huo umeanza majira ya saa kumi alasiri kwa timu zote kucheza kwa tahadhari kwani mchezo huo ulitawaliwa na tambo za Tabora…

Loveness Bernard · Read more

LADHA ZA LIGI KUU NBC ZAREJEA YANGA WAKIWALIZA KAGERA SUGAR

Ladha za Ligi Kuu ya NBC zimerejea rasmi leo Februari 1 kwa mchezo mmoja uliochezwa uwanja wa KMC mkoani Dar es Salaam ambapo timu ya Yanga waliwakaribisha Kagera Sugar. Mchezo ulianza majira ya saa kumi alasiri kwa timu zote kushambuliana kwa kasi huku Yanga wakionekana kuutawala mchezo. Ilimchukua dakika 32 mshambuliaji wa Yanga Clement Mzize…

Loveness Bernard · Read more

HAWA HAPA WAKALI WA NAMBA LIGI KUU YA NBC.

Ligi Kuu ya NBC inatarajiwa kurejea tena Februari 1, 2025 kwa mchezo mmoja kati ya Young Africans na Kagera Sugar saa 10:00 alasiri kwenye uwanja wa KMC Complex. Mpaka Ligi inasimama Desemba 29, 2024 jumla ya mabao 266 yalifungwa huku Mchezaji Elvis Rupia wa Singida Black Stars akiongoza kwa ufungaji akiwa na mabao nane akifuatiwa…

Yahaya Abushehe · Read more

LIGI KUU NBC KUREJEA WIKIENDI .

Ligi Kuu ya NBC ligi ya nne kwa ubora barani Afrika inarejea wikiendi hii febuari 1 baada ya mapumziko ya takribani mwezi mmoja . Ligi hiyo itaanza kwa michezo miwili ya viporo vya mzunguko wa 16 ambavyo ni mechi za Yanga dhidi ya Kagera Sugar Februari 1 katika uwanja wa KMC mkoani Dar es Salaam.…

Loveness Bernard · Read more

STAND YAILIZA KILUVYA,MBUNI YAJIPATA KWA POLISI NBC CHAMPIONSHIP

LIGI ya NBC Championship Mzunguko wa 16 leo imeendelea kwa michezo minne ya mwisho ya mzunguko huo iliyochezwa viwanja mbalimbali nchini kuanzia majira ya saa nne asubuhi na saa kumi jioni. Bigman waliwakaribisha Mbeya City katika uwanja wa Ilulu mkoani Lindi saa nne asubuhi baada ya mchezo huo kuahirishwa kuchezwa jana kutokana na mvua iliyonyesha…

Loveness Bernard · Read more

TMA YAJIPATA KWA GEITA GOLD NBC CHAMPIONSHIP

LIGI ya NBC Championship Mzunguko wa 16 ulianza jana januari 24 kwa michezo ilicho na leo imeendelea kwa mchezo mmoja uliochezwa mkoani Arusha Katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid majira ya saa kumi jioni. Katika mchezo huo timu ya TMA waliwakaribisha Geita Gold ambapo mchezo ulianza kwa timu zote kushambuliana kwa kasi kubwa ambapo mpaka…

Loveness Bernard · Read more

MTIBWA HASHIKIKI NBC CHAMPIONSHIP.

LIGI ya NBC Championship Mzunguko wa 16 ulianza jana Januari 24 kwa michezo mitatu kuchezwa kwenye mikoa mitatu tofauti. Mkoani Mtwara, Mbeya kwanza iliibuka na ushindi wa mabao mawili kwa moja dhidi ya Songea United, ushindi ulioipandisha Mbeya kwanza hadi nafasi ya nne kwenye msimamo ikifikisha alama 30. African Sports ya Tanga iliifunga Cosmopolitan…

Yahaya Abushehe · Read more