News

Announcements, match reports and updates from the Tanzania Premier League Board.

LIGI KUU YA NBC KUCHEZWA ARUSHA, SINGIDA LEO.

LIGI Kuu ya NBC inaendelea leo Februari 7, 2025 kwa michezo miwili kuchezwa kwenye mikoa ya Arusha na Singida kuanzia saa 10:00 Alasiri. Mkoani Arusha Coastal Union itaikaribisha JKT Tanzania kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid huku ikiingia kwenye mchezo huu ikishika nafasi ya 11 ikikusanya alama 18 kwenye michezo 16 na JKT Tanzania ikishika nafasi ya…

Yahaya Abushehe · Read more

DODOMA JIJI YASHINDWA KUTAMBA NYUMBANI.

TIMU ya Dodoma Jiji imepoteza mchezo wake wa kwanza wa Ligi Kuu ya NBC baada ya kurejea kutoka kwenye mapumziko mafupi kwa bao moja kutoka kwa Pamba Jiji ya mkoani Mwanza. Mchezo huo uliokutanisha timu zilizopo chini ya manispaa za jiji ulipigwa kwenye uwanja wa Jamhuri, Dodoma na kushuhudia bao lililofungwa kipindi cha kwanza na…

Honest Mwanitega · Read more

PRISONS YAIDUWAZA MASHUJAA LIGI KUU YA NBC.

TIMU ya Tanzania Prisons imerejea vema kwenye Ligi Kuu ya NBC baada ya kuifunga Mashujaa mabao 2-1 kwenye uwanja wa Sokoine, Mbeya. Mabao ya Prisons yalifungwa na Beno Ngassa mdogo wa nyota wa zamani wa timu ya taifa ya Tanzania Mrisho Ngassa na Meshack Mwamita aliyefunga bao la ushindi kipindi cha pili huku bao la kufutia…

Honest Mwanitega · Read more

FOUNTAIN GATE,SIMBA WATOSHANA NGUVU LIGI KUU NBC.

LIGI Kuu ya NBC imeendelea jana mkoani Manyara ambapo timu ya Fountain Gate Iliwakaribisha timu ya Simba katika uwanja wa Tanzanite Kwaraa majira ya saa kumi alasiri. Mchezo huo ulianza kwa kasi ambapo timu zote zilionekana kushambuliana kwa kasi kubwa huku kila timu ikionyesha nia ya kuzitaka alama tatu muhimu za mchezo huo jambo lilipolekea…

Loveness Bernard · Read more

MTIBWA WABABE WA NAMBA NBC CHAMPIONSHIP MPAKA SASA.

JUMLA ya Michezo 136 kati ya 240 imeshachezwa kwenye Ligi ya Championship ya NBC msimu wa 2024/2025 na kushuhudia jumla ya mabao 297 yakifungwa kwenye michezo hiyo huku Mtibwa Sugar ikiwa kinara kwa kufunga mabao mengi. Mtibwa imefunga jumla ya mabao 31 kwenye michezo 17 mengi zaidi kuliko timu yeyote kwenye Ligi ya Championship ya NBC…

Yahaya Abushehe · Read more

LIGI KUU YA NBC KUCHEZWA VIWANJA VINNE LEO.

LIGI Kuu ya NBC inaendelea kwa mzunguko wa 17 huku mechi nne zikichezwa katika viwanja mbalimbali nchini kuanzia majira ya saa nane mchana. Mchezo wa kwanza utachezwa saa nane mchana katika uwanja wa Jamhuri Dodoma ambapo Dodoma Jiji watawakaribisha Pamba Jiji kutoka jijini Mwanza . Sambamba na mchezo huo Tanzania Prisons “wajelajela” watawakaribisha timu ya Mashujaa “Wana…

Loveness Bernard · Read more

MZIZE,DUBE HAWASHIKIKI LIGI KUU NBC

WASHAMBULIAJI wa Yanga Prince Dube na Clement Mzize wameongeza kasi katika mbio za ufungaji bora baada ya kufung mabao mawili kila mmoja katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya KenGold mchezo uliochezwa leo katika uwanja wa KMC. Licha ya Kocha Mkuu wa Yanga Saed Ramovic kuaga jana ikiwa ni saa chache kuelekea mechi…

Loveness Bernard · Read more

CHIKOLA AWALIZA NAMUNGO LIGI KUU NBC

LIGI Kuu ya NBC imeendelea leo mkoani Tabora kwa mchezo uliozikutanisha timu ya Tabora United dhidi ya timu ya Namungo katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi. Mchezo huo uliochezwa majira ya saa nane mchana ulianza kwa kasi tangu mwanzo kwani dakika ya nne ya mchezo huo mchezaji wa Namungo, Jacob Massawe aliweka mpira wavuni mwa…

Loveness Bernard · Read more

TRANSIT YASHINDWA KUIZUIA STAND NBC CHAMPONSHIP.

LIGI ya NBC ya Championship imeendelea kwa mchezo mmoja uliopigwa uwanja wa Mabatini, Pwani kati ya Transit Camp ya Dar iliyochezea ‘kichapo’ cha mabao 3-0 kutoka kwa Stand United ya Shinyanga. Mchezo ulianza kwa timu zote kushambuliana kwa zamu huku Stand ikitangulia kupata bao mapema lililoipa uongozi hadi kipindi cha kwanza kwanza kinamalizika likifungwa kwa…

Honest Mwanitega · Read more