News

Announcements, match reports and updates from the Tanzania Premier League Board.

NBC CHAMPIONSHIP MZUNGUKO WA 16 KUPIGWA MIKOA MITATU LEO.

MZUNGUKO wa 16 wa Ligi ya Championship ya NBC unaanza kuchezwa leo Januari 24 kwa michezo mitatu kuchezwa kwenye mikoa mitatu tofauti. Mchezo wa kwanza utazikutanisha Mbeya Kwanza dhidi ya Songea United kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona Mkoani Mtwara kuanzia saa 10:00 alasiri. Mchezo wa pili utazikutanisha African Sports dhidi ya Cosmopolitan kwenye uwanja wa…

Yahaya Abushehe · Read more

LIGI KUU NBC YA NNE KWA UBORA AFRIKA

Shirikisho la Kimataifa la Historia na Takwimu za Mpira wa Miguu (IFFHS) limeitangaza Ligi Kuu ya Tanzania (NBC Premier League) kuwa Ligi ya nne kwa ubora barani Afrika na ya 57 duniani kwa mwaka 2024. Ligi hiyo imepanda kwa nafasi mbili kutoka nafasi ya sita mwaka 2023 hadi nafasi ya nne ikizipiku Ligi za Afrika…

Loveness Bernard · Read more

HAWA HAPA WASHINDI WA TUZO ZA NBC DESEMBA.

MSHAMBULIAJI wa Yanga, Clement Mzize amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Desemba wa Ligi Kuu ya NBC huku Kocha wa Yanga Sead Ramovic akichaguliwa kuwa kocha bora wa mwezi huo. Mzize amewashinda Prince Dube wa Yanga na Feisal Salum wa Azam alioingia nao fainali za tuzo hizo baada ya kufunga mabao 4 na kutoa pasi…

Loveness Bernard · Read more

LIGI KUU YA NBC KUREJEA FEBRUARI

BODI ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) inatangaza mabadiliko ya tarehe ya kurejea kwa michezo ya Ligi Kuu ya NBC ambayo hapo awali ilipangwa kuendelea Machi 1, 2025 baada ya kutamatika kwa michuano ya Kombe la Mapinduzi na fainali za mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN). Michezo ya Ligi Kuu ya NBC itarejea katika…

Loveness Bernard · Read more

YANGA MGUU MMOJA NDANI ROBO FAINALI LIGI YA MABINGWA AFRIKA.

BINGWA mtetezi wa Ligi Kuu ya NBC timu ya Yanga imefanikiwa kupata ushindi wa bao moja ugenini dhidi ya AL Hilal na kujiweka kwenye mazingira mazuri ya kufuzu hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Stephane Aziz Ki ndiye aliyepeleka furaha kwa ‘Wananchi’ baada ya kuipatia bao dakika ya saba kwa shuti kali…

Honest Mwanitega · Read more

VINARA WA LIGIKUU YA NBC WAFUZU ROBO FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA.

TIMU ya Simba inayoshiriki Ligi Kuu ya NBC imefanikiwa kufuzu hatua ya robo fainali ya kombe la Shirikisho Afrika baada ya kupata sare ya bao 1-1 ugenini dhidi ya timu ya Bravos de Marquiz ya Angola. Leonel Ateba ndiye alikuwa shujaa wa Simba baada ya kusawazisha bao dakika ya 69 lililoifanya timu yake kufikisha alama…

Honest Mwanitega · Read more

GEITA, STAND VITA YA NAFASI NBC CHAMPIONSHIP LEO.

Ligi ya Championship ya NBC inaendelea leo Januari 12, 2025 kwa michezo miwili kuchezwa katika mikoa ya Geita na Pwani. Mchezo wa kwanza utazikutanisha Kiluvya iliyo nafasi pili kutoka mwisho dhidi ya Mtibwa Sugar vinara wa Ligi ya Championship ya NBC katika uwanja wa Mabatini mkoani Pwani kuanzia saa 10:00 alasiri. Mchezo wa pili…

Yahaya Abushehe · Read more

FEISAL BINGWA WA KUPIKA MABAO LIGI KUU YA NBC.

KIUNGO wa Azam FC Feisal Salum ameendelea kuonyesha ubora aliokuwa nao msimu uliopita ambapo hadi sasa kiungo huyo anaongoza msimamo wa kutoa pasi nyingi zilizozaa mabao (9). Feisal hadi sasa ameongeza pasi mbili za mabao zaidi ya alizimaliza nazo msimu uliopita ambapo alitoa pasi saba huku kinara akiibuka Kipre Junior aliyekuwa akicheza timu moja na…

Honest Mwanitega · Read more

CAMARA KINARA WA KUTORUHUSU MABAO LIGI KUU YA NBC.

Kipa wa Simba Moussa Camara amezidi kujiweka katika nafasi nzuri baada ya kucheza michezo 12 bila kuruhusu bao katika michezo 15 ya Ligi Kuu ya NBC aliyocheza. Golikipa huyo aliyesajiliwa na Simba msimu huu ameonekana kama ‘lulu’ baada ya kuruhusu mabao Matano tu katika michezo yote aliyocheza huku timu yake ikiwa imefunga mabao 31 na…

Loveness Bernard · Read more