News

Announcements, match reports and updates from the Tanzania Premier League Board.

MBEYA, ARUSHA NBC CHAMPIONSHIP ‘KINAWAKA’ LEO.

MICHEZO miwili ya Ligi ya NBC Championship inachezwa leo kwenye mikoa ya Mbeya na Arusha katika muendelezo wa mzunguko wa 19. Mkoani Mbeya KenGold vinara wa NBC Championship itawakabili Mbeya Kwanza inayoshika nafasi ya tano kwenye msimamo saa 8:00 mchana kwenye uwanja wa Sokoine. Mkoani Arusha TMA inayoshika nafasi ya sita na alama 34…

Yahaya Abushehe · Read more

MICHEZO MITATU NBC CHAMPIONSHIP KUPIGWA LEO.

LIGI ya NBC Championship inarejea leo Januari 26 kwa michezo mitatu ya mzunguko wa 19 kuchezwa kwenye mikoa mitatu tofauti. Mapema saa 8:00 mchana Copco itawaalika Stand United kwenye uwanja wa Nyamagana mkoani Mwanza, Copco inashika nafasi ya 15 kwenye msimamo ikicheza jumla ya michezo 18 na kupata alama 13 huku Stand United ikishika…

Yahaya Abushehe · Read more

LIGI KUU YA NBC NAMBA SITA KWA UBORA AFRIKA.

SHIRIKISHO la Kimataifa la Historia na Takwimu za Mpira wa Miguu (IFFHS) limetoa takwimu za Ligi bora duniani huku Ligi Kuu ya NBC Tanzania ikishika namba 6 barani Afrika. Shirikisho hilo limetoa takwimu za ligi 100 ikijumuisha Bara la Afrika, Ulaya, Amerika ya Kusini, Amerika Kaskazini, Asia, Australia na Antaktiki huku Ligi Kuu ya NBC…

Honest Mwanitega · Read more

HAWA HAPA VINARA WA MABAO NBC CHAMPIONSHIP.

Jumla ya mabao 329 yameshafungwa katika michezo 144 sawa na mizunguko 18 ya Ligi ya NBC Championship mpaka kufikia sasa. Edger William wa KenGold ndiye kinara wa upachikaji mabao ndani ya Ligi ya NBC Championship akifunga mabao 15 huku timu yake ikifunga mabao 32. Boban Bogere wa Biashara United ndiye anayefuatia akifunga mabao 13…

Yahaya Abushehe · Read more

KENGOLD YAREJEA KILELENI, NBC CHAMPIONSHIP IKIENDELEA LEO.

LIGI ya NBC Championship imeendelea leo Januari 21 kwa michezo mitatu kupigwa kwenye mikoa mitatu tofauti. Mchezo wa mapema saa 8:00 mchana ulizikutanisha TMA dhidi ya Cosmopolitan kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha na kumalizika kwa sare ya mabao 2-2. Mkoani Mwanza Copco ikawakaribisha Biashara United kwenye uwanja wa CCM Kirumba saa 10:00…

Yahaya Abushehe · Read more

NBC CHAMPIONSHIP MECHI ZOTE MUBASHARA KUPITIA TV3.

MECHI zote za Ligi ya NBC Championship sasa zitarushwa mubashara na mdhamini mwenye haki ya matangazo TV3. TV 3 ambayo inapatikana kwenye chaneli namba 197 (dish) na 137 (antena) kwenye king’amuzi cha Startimes, awali ilikuwa ikirusha baadhi ya michezo lakini baada ya maboresho ya ratiba sasa michezo yote kuonekana mubashara kupitia chaneli hiyo. Hii…

Yahaya Abushehe · Read more

NBC CHAMPIONSHIP HAKUNA MBABE LEO.

MICHEZO miwili ya mzunguko wa 18 ya Ligi ya NBC Championship imechezwa leo na michezo yote kumalizika kwa sare. Mchezo wa kwanza ulizikutanisha Polisi Tanzania dhidi ya Green Warriors saa 8:00 mchana kwenye uwanja wa ushirika, Kilimanjaro na kumalizika kwa suluhu. Saa 10:00 alasiri kwenye uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro FGA Talents ikaikaribisha Transit…

Yahaya Abushehe · Read more

KILIMANJARO, MOROGORO KUSHUHUDIA NBC CHAMPIONSHIP LEO.

Mzunguko wa 18 wa Ligi ya NBC Championship unaanza leo Januari 19 kwa michezo miwili kuchezwa kwenye mikoa miwili tofauti. Mkoani Kilimanjaro Polisi Tanzania watawaalika Green Warriors saa 8:00 mchana kwenye uwanja wa Ushirika. Saa 10:00 alasiri FGA Talents itakuwa mwenyeji wa Transit Camp kwenye uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro. FGA Talents na Transit…

Yahaya Abushehe · Read more

NYOTA LIGI KUU YA NBC WANG’ARA AFCON 23.

MICHUANO ya fainali za mataifa ya Afrika 2023 zinaendelea nchini Ivory Coast katika miji ya Abdijan, korhogo, Bouake, Yamoussoukro na San Pedro. Michuano hii inajumuisha nyota 18 kutoka timu tano zinazoshiriki Ligi Kuu ya NBC. Stephane Aziz Ki na Djigui Diarra ndiyo wachezaji wa kwanza kuiwakilisha Ligi Kuu ya NBC kwenye Fainali hizi za…

Yahaya Abushehe · Read more