News

Announcements, match reports and updates from the Tanzania Premier League Board.

YANGA KUIVAA MASHUJAA LIGI KUU YA NBC LEO.

LIGI Kuu ya NBC inaendelea Leo Februari 8 kwa mchezo mmoja Kati ya Yanga dhidi ya Mashujaa kwenye uwanja wa Azam Complex saa 1:00 usiku. Yanga inaingia kwenye mchezo huu ikiwa na kumbukumbu ya ushindi kwenye mchezo wao uliopita dhidi ya Dodoma Jiji huku Mashujaa ikipoteza kwenye mchezo wao dhidi ya Simba. Yanga ipo…

Yahaya Abushehe · Read more

NBC CHAMPIONSHIP YAPAMBA MOTO.

MZUNGUKO wa 20 ligi ya NBC Championship umemalizika na kushuhudia jumla ya michezo nane ikichezwa huku mabao 22 yakifungwa. KenGold inaendelea kusalia kileleni mwa msimamo ikiwa na alama 43 kwenye michezo 20 huku Pamba na Biashara United zikifuatia zikiwa na alama 43 kila moja zikitofautiana mabao ya kufunga na kufungwa. Ruvu Shooting yenye maskani…

Yahaya Abushehe · Read more

LIGI KUU YA NBC KUENDELEA LEO, MASHUJAA KUJIULIZA KWA SIMBA.

LIGI Kuu ya NBC inaendelea leo Februari 3 kwa mchezo mmoja kupigwa mkoani Kigoma. Mashujaa itaikaribisha Simba kwenye uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma saa 10:00 alasiri. Mashujaa inaingia kwenye mchezo huu ikiwa nafasi ya 15 kwenye msimamo ikijikusanyia alama tisa kwenye michezo 12 huku Simba ikiwa nafasi ya tatu kwenye msimamo ikiwa na…

Yahaya Abushehe · Read more

NBC CHAMPIONSHIP KUPIGWA MIKOA SITA LEO.

LIGI ya NBC Championship mzunguko wa 20 unaanza leo Februari 3 kwa michezo sita kupigwa kwenye mikoa sita tofauti. Mchezo wa mapema saa 8:00 mchana utazikutanisha Stand United dhidi Biashara United kwenye uwanja wa Mwadui Complex mkoani Shinyanga. Mkoani Mbeya KenGold itaikaribisha Mbeya City saa 10:00 alasiri kwenye uwanja wa Sokoine huku KenGold ikiingia…

Yahaya Abushehe · Read more

KAGERA SUGAR, YANGA HAKUNA MBABE.

LIGI KUU ya NBC imerejea leo kwa mchezo mmoja uliopigwa kati ya kagera Sugar na Yanga katika uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera na kumalizika kwa suluhu. Kwa matokeo haya Kagera Sugar inapanda kwa nafasi moja kutoka 14 hadi 13 baada ya kufikisha alama 14 kwenye michezo 14 huku Yanga ikiendelea kusalia nafasi ya 2…

Yahaya Abushehe · Read more

LADHA ZA LIGI KUU YA NBC KUREJEA LEO.

LIGIKUU ya NBC inarejea leo Februari 2 baada ya kusimama kwa takribani siku 40 kupisha fainali za mataifa ya Afrika. Mchezo mmoja utapigwa leo Kagera Sugar ikiikaribisha Yanga kwenye uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera saa 10:00 alasiri. Kagera Sugar inaingia kwenye huu mchezo ikiwa nafasi ya 14 kwenye msimamo baada ya kukusanya alama 13…

Yahaya Abushehe · Read more

‘STAA’ YUPI WA LIGI KUU YA NBC KUMFUATA INONGA ROBO FAINALI LEO ?

KOMBE la Mataifa ya Afrika linaendelea nchini Ivory Coast huku ‘Mastaa’ watatu wa Ligi Kuu ya NBC wakisalia hadi sasa kwenye mashindano hayo. Mashindano hayo yanaendelea leo huku wachezaji wawili wa Yanga Djigui Diarra anaekipiga timu ya taifa ya Mali na Stephane Aziz Ki wa Burkina Faso wakikutana leo kila mmoja akitafuta nafasi ya kucheza…

Honest Mwanitega · Read more

LIGI KUU YA NBC KUREJEA FEBRUARI 2.

BAADA ya kusimama kwa takribani siku 40 kupisha mashindano ya Mataifa ya Afrika yanayoendelea nchini Ivory Coast Ligi Kuu ya NBC inarejea tena Februari 2. Ligi hiyo itarejea kwa mchezo mmoja utakaopigwa saa 10:00 alasiri kwenye uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera kati ya Kagera Sugar na Yanga. Ligi hiyo namba sita kwa ubora Afrika inarejea…

Honest Mwanitega · Read more