News

Announcements, match reports and updates from the Tanzania Premier League Board.

MTIBWA YAANZA NBC CHAMPIONSHIP KIBABE, MBEYA CITY IKIBANWA NYUMBANI.

LIGI ya NBC Championship imeanza rasmi kwa michezo miwili ya ufunguzi ikizihusisha timu za Mtibwa na Green Warriors, Mbeya City na Big Man FC. Mtibwa imeanza Ligi ya NBC Championship kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Green Warriors mabao yote yakifungwa na Raizin Hafidh, mchezo uliochezwa saa 10:00 alasiri kwenye uwanja wa manungu,…

Yahaya Abushehe · Read more

FOUNTAIN GATE YAPAA, KAGERA SUGAR IKIPETA NYUMBANI.

LIGI Kuu ya NBC imeendelea kwa michezo miwili kuchezwa kwenye mikoa ya Tabora na Kagera. Mkoani Tabora, Tabora UTD ilikuwa mwenyeji wa Fountain Gate katika uwanja wa Ali hassan Mwinyi saa 10:00 alasiri na kushuhudia Tabora ikikubali kichapo cha mabao 1-3. Kwa matokeo hayo Fountain Gate imefikisha alama 10 kwenye michezo mitano ambazo zinaipandisha…

Yahaya Abushehe · Read more

LIGI YA CHAMPIONSHIP YA NBC KUANZA LEO.

MSIMU mpya wa Ligi ya Championship ya NBC unatarajiwa kuanza kutimua vumbi leo kwa michezo miwili itakayopigwa kwenye mikoa miwili tofauti. Michezo yote inatarajiwa kuanza saa 10:00 alasiri, Mbeya City itakuwa mwenyeji wa Bigman FC kwenye uwanja wa Sokoine, Mbeya huku Mtibwa Sugar iliyoshuka daraja kutoka Ligi Kuu ya NBC itakuwa mwenyeji wa Green Warriors…

Honest Mwanitega · Read more

AZAM YAITOLEA UVIVU KMC LIGI KUU YA NBC.

TIMU ya Azam FC imefanikiwa kupata ushindi wa kwanza wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya KMC baada ya kuifunga mabao 0-4 kwenye uwanja wa KMC mkoani Dar es Salaam. Bao la kwanza la Azam msimu huu limefungwa na Iddy Seleman kwenye mchezo huo dhidi ya KMC huku mabao mengine yakifungwa na Lusajo Mwaikenda, Nassor…

Honest Mwanitega · Read more

PAMBA, SINGIDA KUKIWASHA MWANZA, COASTAL KUJIULIZA LIGI KUU YA NBC.

BAADA ya KMC kupata ushindi wa kwanza wa Ligi Kuu ya NBC jana dhidi ya KenGold kwa bao moja huku Kagera Sugar ikitoka suluhu na JKT Tanzania leo ligi hiyo inaendelea kwa michezo miwili. Mapema saa 8:00 mchana timu ya Pamba ya Mwanza itakuwa mwenyeji wa Singida BS kwenye uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza. Pamba…

Honest Mwanitega · Read more

COASTAL KUJIULIZA KWA MASHUJAA LEO KWENYE LIGI KUU YA NBC.

BAADA ya Singida Black Stars na Dodoma Jiji kutamba kwenye uwanja wa nyumbani jana kwa ushindi jana timu ya Coastal Union leo itakuwa mwenyeji wa Mashujaa kuzisaka alama tatu muhimu. Coastal iliyochagua kutumia uwanja wa KMC uliopo Dar kama uwanja wa nyumbani kwenye mchezo huu itacheza huku ikipambana kupata ushindi wa kwanza msimu huu dhidi…

Honest Mwanitega · Read more

‘KIVUMBI’ CHA LIGI KUU YA NBC KUENDELEA.

BAADA ya Tabora United na Fountain Gate kupata ushindi hapo jana Ligi Kuu ya NBC inaendelea tena leo kwa michezo miwili itakayopigwa mikoa miwili tofauti. Saa 10:00 alasiri timu ya Singida BS ya Singida itakuwa mwenyeji wa KMC ya Dar kwenye uwanja wa Liti, Singida. Singida imeshinda michezo yote miwili ya kwanza msimu huu iliyocheza…

Honest Mwanitega · Read more

TABORA UTD, FOUNTAIN GATE ZATAKATA NYUMBANI LIGI KUU YA NBC.

MICHEZO miwili ya Ligi Kuu ya NBC imechezwa Septemba 11 katika mikoa ya Tabora na Manyara na kushuhudia timu mwenyeji wa mikoa hiyo Tabora UTD na Fountain Gate zikitakata. Mchezo wa mapema saa 8:00 mchana Tabora UTD iliialika Kagera Sugar kwenye uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora na kumalizika kwa Tabora kushinda kwa bao…

Yahaya Abushehe · Read more

LIGI KUU YA NBC KUENDELEA LEO.

LIGI Kuu ya NBC inatarajiwa kuendelea leo kwa michezo miwili baada ya kusimama kwa takribani siku 13 kupisha michezo ya kimataifa. Mchezo wa kwanza utachezwa saa 8:00 mchana kati ya timu ya Tabora United itakayokuwa nyumbani kuikaribisha Kagera Sugar kwenye uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mkoani Tabora ukiwa mchezo wa kwanza wa Tabora kwenye uwanja…

Honest Mwanitega · Read more