News

Announcements, match reports and updates from the Tanzania Premier League Board.

JKT, PAMBA HAKUNA MBABE LIGI KUU YA NBC

LIGI Kuu ya NBC imeendelea kwa mzunguko wa 14 kuchezwa michezo miwili iliyopigwa mkoani Dar es Salaam na Kagera. Timu ya JKT Tanzania ilikuwa mwenyeji wa Pamba Jiji ya Mwanza katika uwanja wa Isamuhyo, Dar es Salaam saa kumi alasiri na kumalizika kwa suluhu. Katika mchezo huo golikipa wa Pamba Jiji Yona Amos alitangazwa kuwa…

Loveness Bernard · Read more

CHIKOLA BORA LIGI KUU YA NBC NOVEMBA

MSHAMBULIAJI wa Tabora United Offen Chikola amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Novemba wa Ligi Kuu ya NBC huku Kocha wa Azam Rachid Taoussi akichaguliwa kuwa kocha bora wa mwezi huo. Chikola amewashinda Yacouba Sogne wa Tabora United na Moussa Camara wa Simba alioingia nao fainali za tuzo hizo baada ya kufunga mabao 3 katika…

Loveness Bernard · Read more

AZAM YATAMBA NYUMBANI

LIGI Kuu ya NBC jana iliendelea mkoani Dar es salaam kwa mchezo mmoja uliochezwa Uwanja wa Azam Complex na kushuhudia Azam ikishinda 2-1 dhidi yaSingida Black Stars. Kiungo wa Azam Feisal Salum alifungua ukurasa wa mabao kwa kufunga bao dakika ya 38 akipokea pasi kutoka kwa Idd Selemani Nado hivyo Azam kwenda mapumziko wakiwa wanaongoza…

Loveness Bernard · Read more

MOTO ULIWAKA LIGI KUU NBC

LIGI Kuu ya NBC ilirejea kwa kasi mwishoni mwa wiki iliyopita kwa michezo iliyochezwa katika viwanja mbalimbali nchini. Pamba Jiji ya Mwanza ilikuwa mwenyeji wa Simba katika Uwanja wa CCM Kirumba Novemba 22, na Simba kuondoka na alama zote tatu huku mshambuliaji wao Lionel Ateba akitajwa kuwa mchezaji bora wa mchezo huo baada ya kufunga…

Loveness Bernard · Read more

LIGI KUU YA NBC KUREJEA.

LIGI namba sita kwa ubora barani Afrika Ligi Kuu ya NBC inarejea Novemba 22 baada ya mapumziko ya kalenda ya FIFA ambapo ijumaa Pamba Jiji ya Mwanza itakuwa mwenyeji wa Simba ya Dar es Salaam. Pamba wamecheza michezo 11 mpaka sasa huku wakiwa wamevuna alama nane na wakiwa nafasi ya 15 katika msimamo wa Ligi…

Loveness Bernard · Read more

HAPATOSHI NBC CHAMPIONSHIP

Ligi ya NBC Championship inazidi kushika kasi ambapo mizunguko tisa imeshachezwa mpaka sasa kwa timu zote 16 zinazoshiriki ligi hiyo ambayo kila timu imeonekana ikipambana kuhakikisha inapanda daraja msimu ujao. Mtibwa Sugar ndio wanaongoza msimamo wakiwa na alama 20 wakiwa wamefunga mabao 15 na kufungwa manne sambamba na Geita Gold wakiwa na alama 20 huku…

Loveness Bernard · Read more

MTIBWA, TMA, MBEYA CITY WABABE WA MABAO NBC CHAMPIONSHIP.

IKITIMIZA mizunguko tisa tangu kuanza Ligi ya NBC ya Championship inazidi kushika kasi huku timu za Mtibwa Sugar, TMA na Mbeya City zikiongoza kwa kufunga mabao hadi sasa. Hadi sasa timu hizo zimefanikiwa kufunga mabao 15 huku Mtibwa ikiruhusu mabao manne, TMA ikiruhusu nane na Mbeya City ikiruhusu mabao 11. Kiluvya iliyopanda daraja kutoka Ligi…

Honest Mwanitega · Read more

“UGUMU WA LIGI KUU YA NBC UNATUPA CHACHU KUPAMBANA ZAIDI” ANTONY MLIGO.

MCHEZAJI wa Namungo Anthony Mligo amesema kuwa ubora wa Ligi Kuu ya NBC umefanya ligi hiyo kuwa ngumu kutokana na kila timu kupambana kuhakikisha inapata matokeo ya ushindi. Akizungumza wakati wa siku ya kuongea na vyombo vya Habari kwa timu ya Namungo, Mligo amesema kuwa Ligi ya NBC imekuwa ngumu na hili linajidhihirisha ubora wake…

Loveness Bernard · Read more

SIMBA, AZAM TIMU ZILIZORUHUSU MABAO MACHACHE LIGI KUU NBC

Ligi Kuu ya NBC inaendelea kushika kasi ambapo mpaka sasa mizunguko 9, 10 na 11 kwa baadhi ya tmu imeshachezwa. Timu za Simba na Azam ndio timu pekee zilizoruhusu mabao machache mpaka sasa ambapo kila moja imeruhusu mabao matatu tu. Simba imeruhusu mabao hayo katika michezo miwili dhidi ya Yanga ikifungwa goli moja na mchezo…

Loveness Bernard · Read more