News

Announcements, match reports and updates from the Tanzania Premier League Board.

LADHA ZA LIGI KUU KUCHEZWA VIWANJA VITATU

LIGI Kuu ya NBC itaendelea leo kwa mzunguko wa 22 kuanza kuchezwa katika viwanja vitatu tofauti nchini kuanzia saa nane mchana. Mchezo wa kwanza utakaochezwa leo saa nane mchana ni timu ya Fountain Gate itaikaribisha timu ya Tanzania Prisons katika uwanja wa Tanzanite Kwaraa mkoani Manyara majira ya saa nane mchana. Fountain Gate ipo nafasi…

Loveness Bernard · Read more

MZIZIMA ‘DERBY’ HAKUNA MBABE.

HAKUNA Mbabe ndivyo unavyoweza kusema baada ya mchezo wa ‘Derby’ ya mzizima kati ya Simba SC na Azam FC kutamatika kwa sare ya mabao 2-2 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa. Mabao ya Azam FC yamefungwa na Gibrill Sillah na Zidane Sereri huku yale ya Simba SC yakifungwa na Elie Mpanzu na Abdulrazack Hamza. Zidane Sereri…

Yahaya Abushehe · Read more

NANI KUIBUKA MBABE WA MZIZIMA ‘DERBY’ LEO ?

LIGI Kuu ya NBC inaendelea leo Februari 24, 2025 kwa mchezo mmoja wa ‘Derby’ ya Mzizima kati ya Simba SC na Azam FC kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa kuanzia majira ya saa 1:00 usiku. Simba inaingia kwenye mchezo huu ikiwa na alama 50 baada ya michezo yake 19 huku ikifunga mabao 41 na kuruhusu sita…

Yahaya Abushehe · Read more

TAARIFA YA KAMATI YA USIMAMIZI WA LIGI YA BODI YA LIGI KUU

Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) katika kikao chake cha Februari 21, 2025 ilipitia mwenendo na matukio ya Ligi na kufanya maamuzi yafuatayo; Ligi Kuu ya NBC Mechi Namba 140: Mashujaa FC 0-0 Coastal Union Klabu ya Mashujaa ya Kigoma imeadhibiwa kwa kutozwa faini ya Sh. 1,000,000…

Loveness Bernard · Read more

DABI YA MZIZIMA RASMI KWA MKAPA

BODI ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), imebadili uwanja na muda wa kuanza kwa mchezo namba 167 wa Ligi Kuu ya NBC (Simba SC vs Azam FC) ambao ulipangwa kufanyika kwenye uwanja wa KMC Complex Februari 24, 2025 kuanzia saa 10:00 alasiri. Mchezo huo sasa utafanyika kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam kuanzia saa…

Loveness Bernard · Read more

CAMARA HASHIKIKI ‘HATI SAFI’ LIGI KUU NBC

AMESHINDIKANA ndivyo unavyoweza kusema kwa golikipa wa timu ya Simba, Moussa Camara ambae ni kinara wa ‘hati safi’ katika michezo 19 Ligi Kuu ya NBC baada ya kuwaacha mbali wapinzani wake wa karibu. Camara amesajiliwa na Simba katika dirisha kubwa la usajili anaongoza kutokuruhusu mabao ambapo mpaka sasa amekusanya hati safi 15 katika michezo ya…

Loveness Bernard · Read more

MZIZE,AHOUA HAPATOSHI VITA YA UFUNGAJI BORA

VITA ya ufungaji bora inazidi kushika kasi baada ya Kiungo wa Simba, Jean Ahoua, kufikisha mabao 10 sawa na mchambuliaji wa Young Africans, Clement Mzize, ambae ndio kinara wa mabao baada ya kutamatika mzunguko wa 20 wa Ligi Kuu ya NBC. Ahoua ambae awali alikuwa na mabao nane alifanikiwa kufunga mabao mawili ya penati wakati…

Loveness Bernard · Read more

LIGI KUU YA NBC KUTIMUA VUMBI LEO.

BAADA ya timu za KenGold, JKT Tanzania na Dodoma Jiji kuchukua alama tatu baada ya kushinda michezo yao hapo jana Ligi Kuu ya NBC inatarajiwa kuendelea tena leo kwa michezo mitatu itakayopigwa viwanja vitatu tofauti. Mkoani Arusha timu ya Coastal Union iliyopoteza mchezo wake uliopita dhidi ya Pamba Jiji itakuwa mwenyeji wa Azam kwenye uwanja…

Honest Mwanitega · Read more