News

Announcements, match reports and updates from the Tanzania Premier League Board.

ARAJIGA PILATO WA ‘DERBY’ YA KARIAKOO.

BODI ya Ligi Kuu Tanzania leo Februari 5, imetangaza orodha ya maofisa watakaosimamia mchezo wa ‘DERBY’ ya Kariakoo wakiwemo waamuzi wa mchezo huo, Ahmed Arajiga kutoka Manyara aliyeteuliwa kuwa mwamuzi wa kati akisaidiwa na Mohamed Mkono kutoka Tanga na Kassim Mpanga wa Dar es Salaam huku mwamuzi wa akiba akiwa ni Amina Kyando kutoka Morogoro.…

Yahaya Abushehe · Read more

KENGOLD ,MASHUJAA HAPATOSHI SOKOINE LIGI KUU NBC

LIGI Kuu ya NBC inaendelea leo kwa mzunguko wa 23 kuanza rasmi katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya majira ya saa kumi alasiri. Timu ya KenGold ndio mwenyeji wa mchezo huo ikiikaribisha timu ya Mashujaa kutoka Kigoma ambapo timu zote mbili zikitaka alama tatu muhimu. KenGold iko nafasi ya 16 kwenye msimamo wa Ligi Kuu…

Loveness Bernard · Read more

HUKU DIARRA KULE CAMARA MILANGO IPO SALAMA.

Zimesalia siku nne kuelekea kwenye kwenye ‘DERBY’ ya Kariakoo ambapo Young Africans itakuwa mwenyeji wa Simba kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa Machi 8, 2025 kuanzia saa 1:15 usiku. Young Africans na Simba zinaingia kwenye mchezo huu zikiwa ndio timu zilizoruhusu mabao machache zaidi ya kufungwa, Young Africans ikiruhusu tisa (9) huku Simba ikiruhusu mabao nane…

Yahaya Abushehe · Read more

YANGA WAKALI WA MABAO, SIMBA HAWAFUNGIKI KIRAHISI LIGI KUU YA NBC.

ZIMESALIA siku tano (5) pekee kuelekea mchezo wa ‘DERBY’ ya Kariakoo ambapo Young Africans itakuwa mwenyeji wa Simba kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa Jumamosi ya Machi 8, 2025. Yanga inaingia kwenye mchezo huu ikiwa timu iliyofunga mabao mengi zaidi kwenye Ligi Kuu ya NBC msimu huu ikifunga (58) kwenye michezo 22 iliyocheza huku ikiruhusu mabao tisa pekee.…

Yahaya Abushehe · Read more

AZAM,NAMUNGO WAGAWANA ALAMA,PAMBA KUKIWASHA NA YANGA LIGI KUU NBC

LIGI Kuu ya NBC iliendelea jana kwa michezo miwili ya mzunguko wa 22 kuchezwa viwanja viwili jijini Dar es Salaam. Mchezo wa kwanza ulichezwa saa kumi jioni ambapo timu ya JKT Tanzania iliwakaribisha timu ya KenGold kutoka Mbeya katika uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo uliopo Mbweni mkoani Dar es Salaam. Mchezo ulianza kwa kasi ambapo…

Loveness Bernard · Read more

JKT,KEN GOLD HAPATOSHI LEO LIGI KUU YA NBC

LIGI Kuu ya NBC inaendelea kwa michezo miwili inayopigwa mkoani Dar es salaam katika viwanja vya Meja Jenerali Isamuhyo na Azam Complex. JKT Tanzania wazee wa ‘kichapo cha kizalendo’ itawakaribisha Ken Gold ‘wazee wa makarasha’ katika mchezo utakaochezwa saa kumi alasiri. Ikumbukwe kuwa JKT Tanzania ipo nafasi ya sita kwenye msimamo ikiwa imefunga mabao 15…

Loveness Bernard · Read more

FOUNTAIN GATE YAJIPATA,MASHUJAA MAMBO MAGUMU

LIGI Kuu ya NBC jana michezo iliendelea kwa michezo mitatu iliyochezwa mikoa mitatu tofauti Manyara,Singida na Kagera. Fountain Gate iliwakaribisha timu ya Tanzania Prisons katika uwanja wa Tanzanite Kwaraa mchezo uliochezwa majira ya saa nane mchana. Dakika ya 27 Fountain Gate walipata bao kupitia mchezaji wao Amos Kadikilo kwa mkwaju wa penati na ambalo ndio…

Loveness Bernard · Read more

MTIBWA YAISHUSHIA MVUA YA MABAO GEITA, NBC CHAMPIONSHIP IKIENDELEA.

JUMLA ya mabao 13 yamefungwa kwenye michezo mitano (5) ya Ligi ya Championship ya NBC iliyochezwa leo Februari 26, 2025 kwenye mikoa minne tofauti. Mtibwa Sugar ikiwa nyumbani kwake Manungu mkoani Morogoro imeibuka na ushindi mnono wa mabao 5-0 dhidi ya Geita Gold mpinzani wake wa karibu kwenye msimamo wa Ligi ya Championship ya NBC,…

Yahaya Abushehe · Read more

MTIBWA, GEITA VITA YA UONGOZI NBC CHAMPIONSHIP.

JUMLA ya mechi tano (5) zinachezwa leo Februari 26, 2025 kwenye mikoa ya Lindi, Pwani, Morogoro na Arusha huku michezo yote ikianza saa 10:00 alasiri. Mchezo unaosubiriwa kwa hamu hii leo unazikutanisha Mtibwa Sugar dhidi ya Geita Gold kwenye uwanja wa Manungu mkoani Morogoro, Mtibwa inaongoza msimamo wa Ligi ya Championship ya NBC ikiwa na…

Yahaya Abushehe · Read more