News

Announcements, match reports and updates from the Tanzania Premier League Board.

GUNNERS YAUNGANA NA HAUSUNG NBC CHAMPIONSHIP.

HATIMAYE timu ya Gunners ya mkoani Dodoma imeungana na Hausung ya mkoani Njombe kupanda moja kwa moja Ligi ya Championship ya NBC kwa msimu unaofuata wa 2025/2026 baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mapinduzi na kufikisha alama 35 hivyo kuongoza msimamo wa First League kundi B. Baada ya kutamatika kwa Ligi hiyo kinachofuata…

Yahaya Abushehe · Read more

FIRST LEAGUE KUHITIMISHWA LEO.

LIGI ya First League inahitimishwa leo kwa michezo ya Kundi A na B kwa timu zote kundi A na timu sita kundi B kutupa karata zake kuanzia saa 10:00 jioni, Tayari timu ya Hausung ya mkoani Njombe imeshakata tiketi ya moja kwa moja kushiriki Ligi ya championship ya NBC msimu wa 2024/2025 kutoka kundi A…

Yahaya Abushehe · Read more

HAWA HAPA WABABE WA UWANJA WA NYUMBANI LIGI YA CHAMPIONSHIP YA NBC.

LIGI ya Championship ya NBC inazidi kushika kasi ikiwa ni mzunguko wa 24 huku timu nyingi zikionyesha uwezo ambapo kila timu inataka kufuzu kwenda Ligi Kuu ya NBC msimu 2025-26 huku timu za Mtibwa Sugar, Mbeya City, Geita Gold, Mbeya Kwanza na Songea United zikiwa hazijapoteza mchezo wowote nyumbani hadi sasa. Mtibwa Sugar ipo nafasi…

Loveness Bernard · Read more

MOUSSA CAMARA ANA JAMBO LAKE LIGI KUU YA NBC.

IKISALIA mizunguko saba kutamatika kwa Ligi Kuu ya NBC ‘Mlinda lango’ wa timu ya Simba Moussa Pinpin Camara ameendelea kushikilia usukani wa vinara ambao hawajaruhusu mabao kwenye ligi hiyo. Camara hadi sasa amefikisha idadi ya michezo 15 aliyocheza bila kuruhusu nyavu zake kuguswa huku timu yake ikifungwa mabao nane pekee hadi sasa. Golikipa huyo wa…

Honest Mwanitega · Read more

LADHA ZA LIGI KUU YA NBC KUREJEA APRIL MOSI

LIGI Kuu ya NBC inatarajia kurejea mapema mwezi ujao baada ya mapumziko ya takribani wiki mbili kupisha michezo ya kufuzu Fainali za Kombe la Dunia 2026. Kurejea kwa Ligi Kuu ya NBC ni mwanzo wa mzunguko wa 24 huku ikibaki mizunguko takribani sita ligi hiyo kutamatika. April mosi Tabora United itawakaribisha ‘watoto wa Jangwani’ Young…

Loveness Bernard · Read more

AHOUA ‘HACHEKI NA WOWOTE’ LIGI KUU NBC.

JEAN Ahoua wa timu ya Simba ameendelea kuwa na msimu bora wa Ligi Kuu ya NBC hadi sasa baada ya kuhusika kwenye mabao 19 huku timu yake ikisalia na michezo nane kutamatisha msimu. Ahoua aliyesajiliwa na Simba akitokea Asec Mimosa mpaka sasa amehusika katika mabao 19 baada ya kufanikiwa kufunga mabao 12 kutoa pasi zilizozaa…

Loveness Bernard · Read more

NANI KUMFUATA HAUSUNG NBC CHAMPIONSHIP ?

NANI kuungana na Hausung kwenye Ligi ya Championship ya NBC ndiyo swali linalosubiri majibu yake kutoka kundi B la First League ambapo Rhino Rangers, Gunners na Tanesco wanayo nafasi ya kufanya hivyo. Rhino Rangers ya Tabora ina Jumla ya alama 31 kwenye michezo 13 huku Gunners ya Dodoma ikiwa na alama 29 kwenye michezo 12…

Yahaya Abushehe · Read more

NBC CHAMPIONSHIP YAZIDI KUNOGA

Ligi ya Championship ya NBC mzunguko wa 24 umemalizika kwa Mtibwa Sugar kuwa kinara ikiwa na alama 57 na kushika nafasi ya kwanza huku ikifunga mabao 47 na kufungwa mabao 34. Nafasi ya pili inashikwa na Mbeya City yenye alama 52 mabao 48 huku ikifuatiwa na Stand United inayoshika nafasi ya tatu na alama 52…

Cynthia Michael · Read more

MANUNGU TISHIO KWA TIMU NGENI NBC CHAMPIONSHIP.

UWANJA wa Manungu uliopo Mkoani Morogoro umekuwa tishio kwa timu zinazoenda kucheza dhidi ya mwenyeji wa uwanja huo Mtibwa Sugar baada ya timu hiyo kushinda michezo 12 hadi sasa kwenye uwanja huo na kuwa idadi kubwa hadi sasa kwenye Ligi ya NBC Championship. Mtibwa iliongeza idadi ya ushindi wikiendi iliyopita baada ya kutoka nyuma dhidi…

Honest Mwanitega · Read more