News

Announcements, match reports and updates from the Tanzania Premier League Board.

KASEJA AIFUFUA UPYA KAGERA SUGAR

TIMU ya Kagera Sugar imeanza kujipata katika michezo ya Ligi Kuu ya NBC baada ya kushinda mechi tatu walizocheza hivi karibuni chini ya uongozi wa Kocha wao mpya Juma Kaseja ambaye pia ni golikipa aliyecheza kwa mafanikio makubwa timu ya taifa na timu mbalimbali za Ligi Kuu . Kaseja ambae alichukua mikoba kutoka kwa Kocha…

Loveness Bernard · Read more

KEN GOLD ‘HALI TETE’ LIGI KUU YA NBC.

TIMU ya KenGold kutoka mkoani Mbeya imeendelea kujiweka kwenye wakati mgumu wa kushiriki Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2025/26 baada ya kupoteza mchezo wa 14 wa ligi hiyo msimu huu dhidi ya Azam kwa mabao 2-0 kwenye uwanja wa Sokoine, Mbeya. KenGold inayoshika nafasi ya mwisho kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya NBC imepoteza…

Honest Mwanitega · Read more

JKT YASHINDWA KUTAMBA NYUMBANI LIGI KUU YA NBC.

TIMU ya JKT Tanzania yenye ‘maskani’ yake uwanja wa Isamuhyo, Dar es Salaam imeshindwa kutamba kwenye uwanja wake wa nyumbani baada ya kulazimishwa sare ya 2-2 na timu ya Dodoma Jiji. Pamoja na kutangulia kupata bao kupitia kwa nahodha wake Edward Songo JKT ilishindwa kuizuia Dodoma iliyokuwa ikifanya mashambulizi ya mara kwa mara na kusawazisha…

Honest Mwanitega · Read more

FOUNTAIN GATE YASHINDWA ‘KUFURUKUTA’ KWA SINGIDA LIGI KUU YA NBC.

Ligi Kuu ya NBC mzunguko 24 imeendelea huku mchezo uliochezwa mkoani Manyara kati ya Fountain Gate na Singida Black Star ukishuhudia Fountain ikishindwa kutamba na kufungwa mabao 3-0. Dakika ya 29 zilitosha kuipa uongozi Singida Black Star kwa bao la kwanza kupitia mchezaji wake Jonathan Sowah aliyefunga bao lake la 7 tangu kujiunga na miamba…

Cynthia Michael · Read more

PAMBA JIJI YABANWA NYUMBANI LIGI KUU YA NBC.

IKICHEZA mchezo wa tano mfululizo timu ya Pamba Jiji imeshindwa kupata ushindi baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 na timu ya Namungo kwenye uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza. Namungo ilikuwa ya kwanza kufungua ukurasa wa mabao kupitia kwa Jacob Massawe huku Pamba ikisawazisha kupitia kwa Nyota Abdoullaye Camara anayecheza kwa mkopo kutokea timu ya…

Honest Mwanitega · Read more

YANGA YAENDELEA ILIPOISHIA LIGI KUU YA NBC.

VINARA wa Ligi Kuu ya NBC Young Africans imeendelea kugawa ‘dozi’ inapocheza uwanja wa ugenini baada ya kuifunga Tabora United mabao 3-0 kwenye uwanja wa Ally Hassan Mwinyi, Tabora. Mchezo wa jana umeshuhudia wachezaji wa Young Africans Prince Dube na Clement Mzize wakifunga bao moja kila mmoja na wote kufikisha mabao 11 msimu huu huku…

Honest Mwanitega · Read more

LIGI KUU YA NBC KUWAKA VIWANJA VINNE LEO

LADHA za Ligi namba nne kwa ubora barani Afrika zinarejea rasmi leo kwa michezo minne itakayopigwa kwenye viwanja tofauti nchini ikiwa ni baada ya mapumziko ya michuano ya kufuzu Kombe la Dunia 2026. Mchezo wa kwanza utakuwa jijini Mwanza ambapo timu ya Pamba Jiji itakuwa mwenyeji wa timu ya Namungo katika uwanja wa CCM Kirumba…

Loveness Bernard · Read more

MBEYA, STAND VITA YA NAFASI NBC CHAMPIONSHIP LEO.

‘VITA YA NAFASI’ ndivyo unavyoweza kuuita mchezo huu ambapo MBEYA City itaikaribisha Stand United kwenye uwanja wa Sokoine, Mbeya kuanzia saa 10:00 alasiri, kwenye muendelezo wa michezo ya Ligi ya Championship ya NBC. Mbeya City ipo nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi ya Championship ya NBC ikiwa na alama 52 sawa na Stand United…

Yahaya Abushehe · Read more