News

Announcements, match reports and updates from the Tanzania Premier League Board.

STAND, GEITA KUISAKA LIGI KUU YA NBC.

IKITAMATIKA kwa mzunguko wa 30 ligi ya Championship ya NBC na kushuhudia Mtibwa Sugar ikiibuka mabingwa wa ligi hiyo na Mbeya City kupanda daraja timu za Stand United ya Shinyanga na Geita Gold ya Geita bado zina nafasi ya kushiriki Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2025/26. Stand iliyomaliza nafasi ya tatu kwenye msimamo wa…

Honest Mwanitega · Read more

NYASI ‘KUWAKA’ MOTO LIGI KUU YA NBC

LIGI Kuu ya NBC leo inatimua vumbi kwa michezo miwili itakayopigwa kwenye viwanja vya Sokoine, Mbeya na Kaitaba, Kagera. Mchezo wa saa 10:00 alasiri utakuwa kati ya Tanzania Prisons dhidi ya Coastal Union ambapo Prisons inahitaji kushinda mchezo wa leo ili kujiondoa kwenye nafasi ya kucheza michezo ya mtoano. Endapo Prisons inayoshika nafasi ya 14…

Honest Mwanitega · Read more

AHOUA MKALI WA ‘KUCHEKA NA NYAVU’ LIGI KUU YA NBC.

KIUNGO wa timu ya Simba Jean Ahoua ameendelea kujiimarisha kwenye mbio za ufungaji bora baada ya kufikisha mabao 15 ikiwa ni msimu wake wa kwanza tangu ajiunge na timu hiyo kwenye Ligi Kuu ya NBC. Ahoua amefanikiwa kufunga mabao hayo akiwa amecheza mechi 24 kwa jumla ya dakika 1773 katika Ligi Kuu ya NBC msimu…

Loveness Bernard · Read more

COSMOPOLITAN YAAGA NBC CHAMPIONSHIP

TIMU ya Cosmopolitan kutoka Dar es Salaam imeshuka daraja kutoka Ligi ya Championship ya NBC na kuungana na Biashara United ya Mara hivyo rasmi timu hizo zitashiriki ligi ya First League msimu wa 2025/26. Cosmopolitan imeshuka daraja baada ya kukubali kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Songea United kwenye mchezo wa mwisho wa ligi hiyo.…

Honest Mwanitega · Read more

SIMBA ‘YAIBAMIZA’ KMC LIGI KUU NBC

LIGI Kuu ya NBC imeendelea leo kwa mchezo mmoja uliochezwa uwanja wa KMC Complex, mkoani Dar es Salaam kati ya KMC ikiikaribisha timu ya Simba na kushuhudia ‘Mnyama’ akishinda 1-2 ugenini. Mchezo huo ulianza majira ya saa kumi alasiri kwa timu zote kuwa na ari ya kuzitaka alama tatu muhimu KMC ikitaka kujihakikishia nafasi ya…

Loveness Bernard · Read more

MTIBWA SUGAR MABINGWA LIGI YA CHAMPIONSHIP YA NBC 2024/2025.

TIMU ya Mtibwa Sugar ya mkoani Morogoro imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi ya Championship ya NBC msimu wa 2024/2025. Mtibwa Sugar kwenye mchezo wake wa mwisho hii Leo dhidi ya Kiluvya iliyochezwa kwenye uwanja wa Manungu Complex imefanikiwa kuibuka na kushinda wa mabao 2-0 myaliyofungwa na Raizin Hafidh dakika ya 36 na 46 ya mchezo…

Loveness Bernard · Read more

NBC CHAMPIONSHIP KUHITIMISHWA LEO.

PAZIA la Ligi ya Championship ya NBC linafungwa leo Mei 11 kwa michezo nane kupigwa kwenye viwanja nane tofauti kuanzia saa 10:00 alasiri. Michezo ya Leo itamtambulisha bingwa wa Ligi ya Championship ya NBC Kati ya Mtibwa Sugar au Mbeya City pia kujua ni timu gani itaungana na Biashara United kushuka daraja. Mtibwa ili kuwa…

Yahaya Abushehe · Read more

CARGO, KAJUNA ZATAMBA NYUMBANI MTOANO FIRST LEAGUE.

Michezo ya mtoano (PlayOff) kubaki au kupanda ligi ya First League imechezwa Jana Mei 8 ikishuhudiwa timu zilizokuwa nyumbani Cargo ya Dar na Kajuna ya Kigoma zikiibuka na ushindi. Mchezo wa kwanza katika uwanja wa TFF Center – Kigamboni uliishuhudia Cargo ikiibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Tunduru Korosho. Mchezo wa pili mkoani…

Yahaya Abushehe · Read more

AHOUA HASHIKIKI, SIMBA IKIWASHA MOTO LIGI KUU YA NBC

UTAMU wa Ligi namba nne kwa ubora barani Afrika unazidi kukolea timu ya Simba ikiichapa timu ya Pamba Jiji kutoka jijini Mwanza mabao 5-1. Mchezo huo uliopigwa katika uwanja wa KMC uliopo Mwenge mkoani Dar es Salaam ulishuhudia kiungo wa timu ya Simba Jean Ahoua akifunga Mabao matatu (Hat-Trick). ilimchukua dakika 16 kufungua ukurasa wa…

Loveness Bernard · Read more