News

Announcements, match reports and updates from the Tanzania Premier League Board.

TABORA, KMC KUFUNGA MZUNGUKO WA 28 LIGI KUU YA NBC.

MZUNGUKO wa 28 unatarajiwa kukamilika leo kwa mchezo mmoja utakaozikutanisha timu za Tabora United kutoka mkoani Tabora dhidi ya KMC ya Dar es Salaam saa 10:00 alasiri kwenye uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora. KMC itashuka ugenini ikiwa na kumbukumbu mbaya ya kupoteza mchezo wake uliopita dhidi ya Simba kwa mabao 1-2 kwenye uwanja wake…

Honest Mwanitega · Read more

AZAM YAFANYA ‘MAUAJI’ LIGI KUU YA NBC.

TIMU ya Azam kutoka Dar es Salaam imeishushia kipigo kizito Dodoma Jiji cha mabao 5-0 kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliochezwa uwanja wa Azam Complex, Dar. Hiki ni kipigo kikubwa zaidi hadi sasa kwenye mzunguko wa 28 ukisalia mchezo mmoja pekee utakaopigwa leo kukamilisha mzunguko huo. Nahodha wa Azam Lusajo Mwaikenda alikuwa mfano…

Honest Mwanitega · Read more

YOUNG AFRICANS YASHIKILIA ‘USUKANI’ LIGI KUU YA NBC.

LIGI Kuu ya NBC inazidi kushika kasi Iikielekea ukingoni huku timu ya Young Africans ikiendelea ilipoishia baada ya kuichapa Namungo 3-0 kwenye uwanja wa KMC Complex mkoani Dar es Salaam. Ilimchukua dakika 27 kiungo wa Young Africans Aziz Ki kufungua ukurasa wa mabao na dakika nne baadae mshambuliaji wa timu hiyo raia wa Zimbabwe Prince…

Loveness Bernard · Read more

KAGERA SUGAR RASMI NBC CHAMPIONSHIP

TIMU ya Kagera Sugar imeaga rasmi Ligi Kuu ya NBC baada ya timu ya Pamba Jiji kuifunga KenGold 0-2 ugenini na kufikisha alama 30 ambazo haziwezi kufikiwa na Kagera ikiwa itashinda michezo yake miwili iliyosalia. Pamba Jiji ilipata bao lake la kuongoza kipindi cha kwanza lililofungwa na mchezaji Yonta Camara dakika ya 30…

Cynthia Michael · Read more

FOUNTAIN ‘HALI TETE’ LIGI KUU YA NBC.

Ligi Kuu ya NBC imeendelea mzunguko wa 28 JKT Tanzania ikiikaribisha Fountain Gate ya mkoani Manyara kwenye uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo na ‘kuichapa’ mabao 3-1 na kuishusha hadi nafasi ya 13 ya msimamo wa Ligi Kuu ya NBC. Ilimchukua dakika saba pekee Mohamed Bakari kuwaamsha mashabiki wa JKT kwa kuipatia timu yake bao…

Cynthia Michael · Read more

LIGI KUU NBC KAZINI VIWANJA VINNE LEO.

BAADA ya kupigwa michezo miwili jana Ligi Kuu ya NBC inaendelea leo kwa michezo minne ya mzunguko wa 28 katika viwanja vinne tofauti . Mchezo wa kwanza utapigwa majira ya saa 8:00 mchana katika uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo uliopo Mbweni Dar es Salaam ambapo JKT Tanzania itaikaribisha timu ya Fountain Gate kutoka Manyara. Saa…

Loveness Bernard · Read more

KAGERA SUGAR ‘HATIHATI’ KUSHIRIKI LIGI KUU YA NBC MSIMU UJAO.

MATUMAINI ya wapenzi na mashabiki wa timu ya Kagera Sugar kusalia Ligi Kuu ya NBC yamezidi kufifia baada ya kufungwa na timu ya Mashujaa katika uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera jana kwa bao 1-0. Timu hiyo imeshacheza michezo 28 ya Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2024/25 na kufanikiwa kuvuna alama 22 ikifunga mabao 22…

Loveness Bernard · Read more

PRISONS YATAKATA SOKOINE LIGI KUU YA NBC

LIGI Kuu ya NBC imeendelea mkoani Mbeya ambapo timu ya Tanzania Prisons iliikaribisha timu ya Coastal Union katika uwanja wa Sokoine na kukusanya alama zote tatu baada ya ushindi wa 2-1. Mchezo huo ulianza saa 10:00 alasiri timu zote zilionyesha ari ya kupambania alama tatu muhimu ili kuweza kujiweka katika mazingira ya kusalia Ligi Kuu…

Loveness Bernard · Read more

CAMARA MKALI WA ‘HATI SAFI’ LIGI KUU YA NBC.

GOLIKIPA wa timu ya Simba, Moussa Camara ameendeleza moto wake wa kuongoza kwa kuwa na hati safi nyingi kuliko magolikipa wengine wa timu za Ligi Kuu ya NBC akiwa hajaruhusu bao kwenye michezo 16 akiwa kwenye msimu wa kwanza ndani ya Simba. Camara mpaka sasa amecheza michezo 24 sawa na dakika 2160 huku timu yake…

Loveness Bernard · Read more