News

Announcements, match reports and updates from the Tanzania Premier League Board.

PACOME ,HAMDI WABEBA TUZO ZA JUNI LIGI KUU YA NBC.

KIUNGO wa timu ya Young Africans, Peodoh Pacome Zouzoua amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa mwezi Juni wa Ligi Kuu ya NBC msimu wa mwaka 2024/2025, huku Miloud Hamdi wa Yanga, akichaguliwa kuwa Kocha Bora wa ligi hiyo kwa mwezi huo. Pacome alionesha kiwango kizuri chenye mwendelezo akiwashinda Clatous Chama wa Yanga na Kibu Denis wa…

Loveness Bernard · Read more

BODI YA LIGI KUU TANZANIA (TPLB) KUPOKEA MAONI YA MABORESHO YA KANUNI ZA LIGI

BODI ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) inaujulisha umma kuwa leo Julai 11, 2025 imeanza rasmi kupokea maoni ya maboresho ya Kanuni za Ligi kuelekea msimu wa 2025/2026. Zoezi hilo la kupokea maoni litafanyika kwa kipindi cha majuma matatu ambapo litafungwarasmi Agosti 1, 2025. Maoni ya maboresho ya kanuni yawasilishwe TPLB kwa kupitia njia zifuatazo; i.…

Loveness Bernard · Read more

STAND UNITED, FOUNTAIN GATE NI VITA YA KUCHEZA LIGI KUU YA NBC.

HATUA ya mtoano wa nani kusalia ama kupanda Ligi Kuu ya NBC inaendelea kesho kwa mchezo mmoja kati ya Stand United ya mkoani Shinyanga itakayokuwa mwenyeji wa timu ya Fountain Gate kwenye uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga. Mchezo huo utakaopigwa saa kumi alasiri utakuwa muhimu kwa timu zote ili kujihakikishia kucheza kwenye ligi namba…

Loveness Bernard · Read more

PRISONS UHAKIKA LIGI KUU NBC 2025/26.

TIMU ya Tanzania Prisons imefanikiwa kusalia Ligi Kuu ya NBC baada ya kuifunga timu ya Fountain Gate 3-1 katika mchezo uliochezwa uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya. Ilimchukua dakika saba mchezaji wa Tanzania Prisons,Beno Ngasa kufungua ukurasa wa mabao huku mchezaji wa Fountain Gate Laurian Makame akisawazisha dakika ya 27 kabla ya Ezekiel Mwashilindi kuiongezea Prisons…

Loveness Bernard · Read more

NI VITA YA NANI KUBAKI LIGI KUU YA NBC SOKOINE LEO.

MCHEZO wa pili wa hatua ya mtoano kati ya Tanzania Prisons dhidi ya Fountain Gate unatarajiwa kupigwa leo kwenye uwanja wa Sokoine, Mbeya kutafuta timu itakayosalia kwenye Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2025/2026. Huu ni mchezo wa mwisho kwa timu zinazoshiriki Ligi Kuu ya NBC kukutana msimu huu baada ya kumaliza kwenye nafasi ya…

Loveness Bernard · Read more

YOUNG AFRICANS MABINGWA LIGI KUU YA NBC 2024/2025

PAZIA la Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2024/2025 limefungwa rasmi jana katika mchezo wa dabi ya Kariakoo ambapo timu ya Young Africans iliibuka na ushindi. Katika mchezo ulichezwa majira ya saa kumi na moja jioni uwanja wa Benjamin Mkapa timu ya Yanga iliifunga timu ya Simba mabao 2-0 yaliyofungwa na wachezaji Pacome Zouzoa na…

Loveness Bernard · Read more

NI VITA YA UBINGWA ‘DERBY’ YA KARIAKOO LEO.

‘DERBY YA MAAMUZI’ ndivyo unavyoweza kuuita mchezo wa watani wa Jadi ‘Kariakoo Derby’ ndani ya Ligi Kuu ya NBC unachezwa leo saa 11:00 jioni kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es salaam. Huu ni mchezo wa kufunga Pazia la Ligi Kuu ya NBC kwa msimu wa 2024/2025 lakini pia ndio mchezo utakaotoa Bingwa wa…

Yahaya Abushehe · Read more

‘PILATO’ WA DABI YA KARIAKOO HUYU HAPA.

RAIA wa Misri Amin Mohamed Amin ndiye atakayechezesha mchezo wa Young Africans dhidi ya Simba maarufu kama ‘Kariakoo Dabi’ Juni 25 kwenye uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam. Ikiwa Yanga itashinda mchezo huo au kutoa sare ya aina yoyote itaibuka mshindi wa kombe la ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2024/2025 na ikiwa…

Loveness Bernard · Read more

VIWANJA NANE KAZINI LEO LIGI KUU YA NBC.

LIGI Kuu ya NBC inatimua ‘vumbi’ leo kwenye viwanja nane tofauti ikiwa ni michezo ya kukamilisha mzunguko wa 30 wa ligi hiyo msimu wa 2024/25. Macho na masikio yatakuwa zaidi kwa ‘Vigogo’ wa ligi hiyo timu za Yanga na Simba zilizopishana alama moja pekee huku timu hizo zikiwa nyumbani kwenye michezo yao ya leo. Young…

Honest Mwanitega · Read more