News

Announcements, match reports and updates from the Tanzania Premier League Board.

AZAM YATAKATA KMC COMPLEX.

TIMU ya Azam imeendeleza ubabe wake dhidi ya timu ya KMC baada ya kuifunga 0-2 katika mchezo uliopigwa leo kwenye uwanja wa KMC Complex, Dar es Salaam. Katika mchezo huo timu zote zilikuwa zikiutaka mchezo na zilishambuliana kwa kasi licha ya Azam kuutawala mchezo huo lakini hadi dakika 45 zinatamatika hakuna aliyefanikiwa kuguza nyavu za…

Loveness Bernard · Read more

SINGIDA YAONGEZA MAUMIVU KWA MTIBWA.

SINGIDA Black Stars imejipata baada ya kuifunga timu ya Mtibwa Sugar mabao 3-1 kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa leo katika uwanja wa Jamhuri Dodoma majira ya saa nane mchana. Iliwachukua dakika tano pekee Singida kufungua ukurasa wa mabao kupitia mchezaji wao Nduhumwe Mosi na dakika ya 16 Horso Muaku aliiongezea timu hiyo…

Loveness Bernard · Read more

MIKOA SABA KUNOGESHA LADHA ZA NBC CHAMPIONSHIP LEO

Ladha za NBC Championship zinaendelea Leo, Februari 22, 2025, ambapo pazia la mzunguko wa 19 wa Ligi hiyo linafunguliwa rasmi kwa michezo saba itakayochezwa katika mikoa saba tofauti nchini. Kuanzia saa 10:00 alasiri, kila timu ikisaka alama tatu zenye uzito wa dhahabu katika safari ya kutimiza malengo yake. Mbeya Kwanza vs Transit Camp Mchezo unaovuta…

Yahaya Abushehe · Read more

HUKU NBC CHAMPIONSHIP ‘BOLI’ LINATEMBEA.

Baada ya kuchezwa kwa mizunguko 18 ya Ligi ya Championship ya NBC, jumla ya mabao 325 yamefungwa katika michezo 140 iliyochezwa hadi sasa, hali inayoonesha ushindani mkubwa miongoni mwa timu shiriki. Mbeya Kwanza wanaongoza kwa ufungaji wa mabao, wakiwa wamefumania nyavu mara 37 huku wakiruhusu mabao 18. Kagera Sugar wanafuatia kwa karibu, wakiwa wamefunga mabao 33…

Yahaya Abushehe · Read more

DODOMA JIJI WAJIPATA JAMHURI

Timu ya Dodoma Jiji imejipata katika uwanja wake wa nyumbani wa Jamhuri baada ya kuhakikisha wanashinda kila mchezo wawapo hapo. Dodoma ambayo imecheza na timu ya TRA United jana imefanikiwa kushinda michezo minne katika uwanja huo,sare mbili na huku ikipoteza mchezo mmoja tu katika michezo saba ambayo timu hiyo imecheza uwanjani hapo. Katika mchezo wa…

Loveness Bernard · Read more

MAHESABU MAKALI NBC CHAMPIONSHIP IKIINGIA MZUNGUKO WA 18.

Mzunguko wa 18 wa NBC Championship unaanza leo ukiwa umebeba presha na mahesabu makali kwa kila timu. Kadri msimu unavyoelekea hatua ya mwisho, kila alama imekuwa ya thamani kubwa katika mbio za kupanda Ligi Kuu ya NBC na vita ya kujiokoa kushuka daraja. Timu nne zilizo juu ya msimamo Geita Gold, Kagera Sugar, Mbeya Kwanza…

Yahaya Abushehe · Read more

COASTAL, PAMBA ZATAMBA LIGI KUU YA NBC.

TIMU ya Coastal Union imeonyesha ubabe ugenini katika Uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya baada ya kuichapa Tanzania Prisons mabao 4-1. Mchezo ulianza kwa kasi Coastal Union wakipata bao la mapema zaidi kwenye Ligi Kuu ya NBC msimu huu lililofungwa sekunde ya 58 kupitia kwa Bakari Msimu na dakika tatu kabla ya mchezo kwenda mapumziko…

Cynthia Michael · Read more

DODOMA YAPANDA NAFASI YA SITA LIGI KUU YA NBC.

DODOMA Jiji imeendelea kuonyesha makali yake kwenye Ligi Kuu ya NBC baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2–1 dhidi ya KMC katika mchezo uliochezwa Jijini Dodoma kwenye uwanja wa Jamhuri. Bao la kwanza la Dodoma Jiji lilifungwa dakika ya 43 na Faraji Kayanda na Kipindi cha kwanza kumalizika Dodoma ikiwa mbele kwa bao…

Cynthia Michael · Read more

LIGI KUU YA NBC ‘KUCHANJA MBUGA’ LEO.

LIGI Kuu ya NBC itaendelea leo kwa michezo miwili itakayochezwa katika mikoa ya Mwanza kwenye uwanja wa CCM Kirumba na Mbeya kwenye uwanja wa Sokoine. Mchezo wa kwanza utakuwa saa 8:00 mchana ambapo timu ya Pamba Jiji ya Mwanza itaialika timu ya Coastal Union ya Tanga katika ‘dimba’ la Kirumba. Pamba Jiji inashika nafasi ya…

Loveness Bernard · Read more