News

Announcements, match reports and updates from the Tanzania Premier League Board.

MTIBWA HAIKAMATIKI,JKT YAREJEA KILELENI LIGI KUU YA NBC.

LIGI Kuu ya NBC imeendelea kwa michezo miwili iliyochezwa mkoani Dodoma kwenye uwanja wa Jamhuri na jiji Dar es saalam katika uwanja wa Mej. Jen Isamuhyo. Mchezo wa Kwanza uliopigwa saa kumi alasiri kati ya Mtibwa Sugar na Tanzania Prisons na kushuhudia Mtibwa sugar ikiibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Tanzania Prisons.…

Cynthia Michael · Read more

COASTAL, TRA HAKUNA MBABE MKWAKWANI.

TIMU ya Coastal union imeshindwa kupata ushindi nyumbani kwenye mchezo wa pili mfululizo baada ya kulazimishwa sare ya bao moja na TRA kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya NBC katika uwanja wa Mkwakwani, Tanga. Coastal union ilikuwa ya kwanza kupata bao dakika ya 35 kupitia kwa Shiza Kichuya aliyesajiliwa kwenye dirisha dogo la usajili…

Cynthia Michael · Read more

NI VITA YA NAFASI NBC CHAMPIONSHIP LEO

LIGI ya Championship ya NBC inaendelea leo kwa michezo miwili mikubwa yenye uzito wa kipekee katika kupambania nafasi za juu na kuepuka hatari ya kushuka daraja. Katika mchezo unaovuta hisia za mashabiki wengi, Transit Camp itaialika Kagera Sugar kwenye uwanja wa Filbert Bayi mkoani Pwani, huku mchezo mwingine ukizikutanisha Hausung na African Sports katika uwanja…

Yahaya Abushehe · Read more

AZAM HAIJAPOTEZA MCHEZO KWENYE LIGI KUU YA NBC.

LIGI kuu ya NBC imeendelea kwa timu ya Azam kuwakaribisha TRA United katika dimba la Azam Complex kwenye pambano lililokuwa na ushindani mkubwa na Azam ikiibuka mbabe kwa kushinda mabao 2-0. Azam wakicheza nyumbani walianza mchezo kwa kasi wakitawala umiliki wa mpira na kutengeneza nafasi zilizozaa matunda baada ya Jean Ngite kufunga bao la kuongoza…

Cynthia Michael · Read more

VIWANJA VIWILI KUWAKA MOTO LIGI KUU YA NBC LEO.

LIGI Kuu ya NBC leo itaendelea mkoani Dar es Salaam katika viwanja viwili ambapo timu ya Simba itakuwa mwenyeji wa Mashujaa katika uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo majira ya saa 10:00 alasiri huku timu ya Azam ikiwaalika TRA katika uwanja wa Azam Complex Chamazi saa 1:00 usiku. Simba ipo nafasi ya sita katika msimamo wa…

Loveness Bernard · Read more

YOUNG AFRICANS YAREJEA KILELENI LIGI KUU YA NBC.

TIMU ya Young Africans imeendelea kuonyesha kwanini inaiwakilisha nchi kwenye mashindano ya Afrika baada ya kushinda 3-1 dhidi ya Dodoma Jiji na kukwea hadi nafasi ya kwanza ya msimamo wa Ligi Kuu ya NBC. Young Africans iliyokuwa ya kwanza kuruhusu bao dakika nne kabla ya kipindi cha kwanza kutamatika kupitia kwa Edgar William haikukata tamaa…

Honest Mwanitega · Read more

MTIBWA YAENDELEZA MOTO LIGI KUU YA NBC

TIMU ya Mtibwa Sugar imefanikiwa kuondoka na alama tatu muhimu baada ya kuifunga Pamba Jiji bao moja katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliochewa katika dimba la Jamhuri mkoani Dodoma. Mchezo huo uliokuwa mkali tangu mwanzo ulishuhudia timu zote zikicheza kwa tahadhari kubwa huku kila moja ikilenga kutumia vizuri nafasi zilizojitokeza ingawa wababe hao…

Cynthia Michael · Read more

DUKE,PEDRO WANG’ARA TUZO ZA DISEMBA

MCHEZAJI Duke Abuya wa Klabu ya Young Africans, amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa mwezi Disemba wa Ligi Kuu ya NBC msimu wa mwaka 2025/26, huku Pedro Goncalves pia wa Young Africans akichaguliwa kuwa Kocha Bora wa Ligi hiyo kwa mwezi huo. Duke alionesha kiwango kizuri chenye mwendelezo akiisaidia timu yake kushinda michezo miwili iliyocheza mwezi…

Loveness Bernard · Read more

DODOMA JIJI, PRISONS KUUMANA LEO LIGI KUU YA NBC.

TIMU ya Dodoma Jiji itaikaribisha Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC utakaochezwa leo majira ya saa 1:00 usiku kwenye uwanja wa Jamhuri, Dodoma. Mchezo huo ni muhimu kwa timu zote mbili kwani zinapambana kujinasua ‘mkiani’ Dodoma Jiji ikiwa nafasi ya 15 katika msimamo wa Ligi Kuu ya NBC baada ya kucheza michezo…

Loveness Bernard · Read more