News

Announcements, match reports and updates from the Tanzania Premier League Board.

SINGIDA YATAMBA UGENINI, DAR ‘DERBY’ HAKUNA MBABE LIGI KUU YA NBC.

LIGI Kuu ya NBC imeendelea kwa timu ya Singida Black Stars kupata ushindi mnono wa mabao 4–1 dhidi ya Mbeya City ugenini katika mchezo uliochezwa mkoani Manyara kwenye uwanja wa Tanzanite Kwaraa, Manyara. Mbeya City ilianza vizuri mchezo na kupata bao la kuongoza dakika ya 14 kupitia kwa mshambuliaji Vitalis Mayanga. Hata hivyo, Singida…

Cynthia Michael · Read more

MAHESABU MAKALI ‘DAR DERBY’ LIGI KUU YA NBC LEO.

Ni vita ya mahesabu makali kwenye Mchezo wa ‘Derby’ ya Dar es salaam leo Machi 15, 2026 ambapo Azam FC itaialika Young Africans kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa saa 2:30 usiku. Azam FC na Young Africans ndio timu pekee kwenye Ligi Kuu ya NBC 2025/2026 ambazo hazijapoteza mchezo wowote hadi sasa katika michezo 13…

Yahaya Abushehe · Read more

YOUNG AFRICANS HAIKAMATIKI LIGI KUU YA NBC.

TIMU ya Young Africans ‘Wananchi’ imezidi kuchanja mbuga kwenye mbio za kuwania ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC baada ya kushinda mchezo wa 11 Kwenye michezo 13 ikiwa haijapoteza hata mmoja na kutoa sare miwili pekee. ’Wananchi’ wameongeza ushindi huo baada ya kuifunga Tanzania Prisons iliyokuwa mwenyeji wa mchezo huo uliopigwa uwanja wa Jamhuri, Dodoma…

Honest Mwanitega · Read more

TRA, SIMBA, AZAM ZAGAWA ‘VICHAPO’ LIGI KUU YA NBC.

BAADA ya kuifunga Fountain Gate mabao 4-1 ugenini timu ya TRA imeshinda mchezo wa pili mfululizo wa Ligi Kuu ya NBC baada ya kuifunga Namungo mabao 2-0 katika uwanja wa Black Rhino uliopo wilaya ya Karatu mkoani Arusha. Mabao ya Chamou Karaboue na Joseph Akandwanaho yalitosha kuwapa furaha ‘walipa kodi’ huku yakipeleka huzuni na vilio…

Honest Mwanitega · Read more

MICHEZO MITATU KUPIGWA LEO LIGI KUU YA NBC

Ligi Kuu ya NBC inaendelea kutimua vumbi leo, Machi 11, 2026, ambapo jumla ya michezo mitatu itapigwa katika mikoa ya Arusha, Singida na Dodoma, huku timu mbalimbali zikiingia uwanjani kusaka alama muhimu katika mbio za msimamo wa ligi. Mchezo wa mapema utapigwa katika Uwanja wa Black Rhino, Karatu mkoani Arusha, ambapo TRA United itakuwa mwenyeji…

Yahaya Abushehe · Read more

SINGIDA YATAKATA, PAMBA IKIBANWA NYUMBANI LIGI KUU YA NBC.

LIGI Kuu ya NBC imeendeleza burudani ya aina yake huku mashabiki wakishuhudia ushindi mwembamba wa bao moja kwa Singida Black Stars dhidi ya Coastal na sare ya kusisimua ya mabao 2-2 kwa Pamba Jiji dhidi ya Azam FC. Katika mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa airtel mkoani singida, Singida Black Stars waliikaribisha Coastal union na…

Cynthia Michael · Read more

DERBY YA KIHISTORIA YA LIGI KUU YA NBC KUPIGWA ZANZIBAR LEO.

Tulihesabu miezi, tukahesabu wiki, tukahesabu siku na sasa tunahesabu masaa kuelekea mchezo mkubwa wa Kariakoo Derby kati ya Young Africans SC na Simba SC utakaopigwa katika dimba la Amaan, visiwani Zanzibar kwenye mpambano wa kusisimua utakaochezwa kuanzia majira ya saa 2:15 usiku leo Machi Mosi. Hii ni mara ya kwanza katika historia ya Ligi Kuu…

Yahaya Abushehe · Read more

SIMBA YAILIZA PRISONS LIGI KUU YA NBC.

TIMU ya Simba imeipa maumivu timu ya Tanzania Prisons baada ya kuifunga mabao 0-2 kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliochezwa uwanja wa Jamhuri Dodoma. Mchezo huo uliokuwa muhimu kwa timu zote ambapo Prisons ikitafuta nafasi ya kujitoka katika eneo la hatari huku Simba ikiwa katika harakati za kujiimarisha na kusogea juu zaidi kwenye…

Loveness Bernard · Read more

YOUNG AFRICANS HAIKAMATIKI LIGI KUU YA NBC.

TIMU ya Young Africans imefanikiwa kuifunga timu ya Namungo bao moja kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliochezwa kwenye uwanja wa Majaliwa mkoani Lindi. Mchezo ulianza kwa timu zote kushambuliana kwa kasi kubwa kuhakikisha wanachukua alama tatu za Ligi Kuu ya NBC ili kujiweka katika nafasi nzuri kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu.…

Loveness Bernard · Read more