News

Announcements, match reports and updates from the Tanzania Premier League Board.

MASHUJAA, YOUNG AFRICANS, NAMUNGO, VITANI LEO LIGI KUU YA NBC.

VIWANJA vitatu vya Ligi Kuu NBC vinaendelea kutoa burudani leo kwa ratiba ya michezo mitatu inayotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa huku kila timu ikihitaji alama kwa malengo tofauti msimu huu. Macho mengi yataelekezwa katika viwanja vya Lake Tanganyika, Kigoma, KMC Complex, Dar es Salaam na Majaliwa, Lindi ambako mapambano ya kibingwa yanayohusisha vita ya nafasi…

Honest Mwanitega · Read more

DODOMA JIJI, MBEYA CITY ZAWASHA MOTO LIGI KUU YA NBC.

LIGI Kuu NBC imeendelea jana kwa michezo miwili iliyotoa burudani ya viwango ambapo Dodoma Jiji iliichapa Fountain Gate mabao 3-0, huku Mbeya City ikiibuka na ushindi wa kusisimua wa 3-2 dhidi ya KMC. Katika mchezo uliopigwa Airtel Stadium, Singida, wenyeji Dodoma Jiji walionyesha ubora mkubwa hasa kipindi cha pili na kuondoka na alama tatu muhimu…

Honest Mwanitega · Read more

SIMBA, COASTAL KUONYESHANA UBABE LEO LIGI KUU YA NBC.

LIGI Kuu ya NBC itaendelea tena mkoani Dar es Salaam leo ambapo timu ya Simba itaikaribisha timu ya Coastal Union katika uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo saa 1:00 usiku. Kila timu imejiandaa vyema ikizitaka alama zote tatu ili kujiweka katika nafasi nzuri ambapo Simba inataka kujihakikishia iko kwenye mbio za ubingwa huku Coastal Union ikitaka…

Loveness Bernard · Read more

AZAM YAONGEZA PRESHA KWENYE ‘KILELE’ CHA LIGI KUU YA NBC.

TIMU ya Azam imeonyesha ubora na ukomavu mkubwa baada ya kuibuka na ushindi muhimu wa mabao 2-1 dhidi ya Singida Black Stars kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa Airtel Stadium, Singida. Baada ya kutoka sare mbili mfululizo bila kufungana, kikosi hicho cha kocha Florent Ibenge kilirejea kwa nguvu na kuonyesha dhamira ya kupambania…

Honest Mwanitega · Read more

LIGI KUU YA NBC KUREJEA LEO.

LIGI Kuu ya NBC inarejea leo baada ya mapumziko ya michezo ya kalenda ya Fifa ambapo timu ya Singida Black Stars itaikaribisha timu ya Azam katika uwanja wa Airtel mkoani Singida saa 10:00 alasiri. Mchezo huo ni muhimu kwa timu zote kwani zinatafuta alama tatu muhimu ili kujiweka katika nafasi nzuri ya mbio za ubingwa…

Loveness Bernard · Read more

NBC CHAMPIONSHIP ‘YAFUKUTA’ MZUNGUKO WA 21.

Ligi ya NBC Championship imetimiza mzunguko wa 21 huku ushindani ukizidi kupamba moto, timu zikionyesha wazi dhamira ya kupigania kupanda daraja kwenda Ligi Kuu ya NBC msimu ujao na nyingine zikipambana kusalia ligi hiyo msimu ujao. Katika hatua hii ya ligi, kila alama imekuwa ya thamani kubwa, huku timu za juu ambazo ni Geita Gold,…

Honest Mwanitega · Read more