News

Announcements, match reports and updates from the Tanzania Premier League Board.

NBC CHAMPIONSHIP 2025/26 YAFIKA TAMATI.

TAMATI ya msimu wa NBC Championship 2025/26 imefika jana huku Geita Gold wakitangazwa mabingwa wa ligi hiyo baada ya kumaliza msimu wakiwa na alama 77 yakiwa mafanikio yaliyowawezesha pia kupanda kushiriki Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2026/27. Sambamba na Geita Gold, Kagera Sugar pia wamefanikiwa kurejea Ligi Kuu ya NBC baada ya kumaliza…

Cynthia Michael · Read more

PAMBA, YANGA, PRISONS ZATEMBEZA ‘DOZI’ LIGI KUU YA NBC.

Michezo mitatu ya raundi ya 27 ya Ligi Kuu ya NBC imechezwa jana katika viwanja tofauti huku mechi zote zikichezwa muda mmoja wa saa 10:00 alasiri huku Pamba Jiji , Yanga na Tanzania Prisons zikiibuka na ushindi muhimu. Katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, Pamba Jiji imepata ushindi mnono kwa kuichapa Mtibwa Sugar…

Cynthia Michael · Read more

PAZIA LA FIRST LEAGUE LAFUNGWA.

Pazia la First League limefungwa jana kwa timu ya Rhino Rangers ya Tabora kufanikiwa kutwaa ubingwa wa First League msimu wa 2025/26 baada ya kuibuka na ushindi wa mikwaju ya penalti 4-2 dhidi ya Bandari kufuatia sare ya mabao 2-2 ndani ya dakika 90 za mchezo wa fainali uliopigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar.…

Cynthia Michael · Read more

MPANZU AIBEBA SIMBA,NDUMUMWE AKIWEKA REKODI MPYA LIGI KUU YA NBC.

Timu ya Simba imeendelea kuweka presha katika mbio za Ligi Kuu ya NBC baada ya kuibuka na ushindi mwembamba wa bao 1-0 ugenini dhidi ya Mbeya City katika mchezo uliochezwa jana mkoani Mbeya kwenye uwanja wa sokoine. Bao pekee la mchezo lilifungwa na Elie Mpanzu dakika ya 43, akimalizia vyema shambulizi la Simba na kuwapa…

Cynthia Michael · Read more

AZAM COMPLEX KUPAMBWA NA FAINALI YA FIRST LEAGUE LEO.

Mabingwa wa makundi ya Ligi ya First League kutoka kundi A na B msimu wa 2025/26, Rhino Rangers waliokuwa kundi B na Bandari Tanzania walikuwa kundi A , leo Juni 17, 2026, watashuka dimbani katika mchezo wa fainali wa kumtafuta bingwa wa jumla wa Ligi ya First League. Mchezo huo utachezwa kwenye Uwanja wa…

Cynthia Michael · Read more

HAKUNA MBABE RUANGWA, AZAM IKIJIIMARISHA LIGI KUU YA NBC.

Namungo na TRA United zimeshindwa kutambiana nguvu baada ya kutoka sare ya bila kufungana katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliochezwa leo majira ya saa 10: 00 alasiri uwanja wa Majaliwa mkoani Lindi. Mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa uliwashuhudia pande zote zikitengeneza nafasi kadhaa za kufunga, lakini uimara wa safu…

Cynthia Michael · Read more

MICHEZO MIWILI KUPAMBA LIGI KUU YA NBC LEO.

MICHEZO miwili ya Ligi Kuu ya NBC itaendelea leo, Juni 16 huku timu zikisaka alama muhimu katika hatua za mwisho wa msimu kuhakikisha zinafikia malengo yao ya msimu huu. Mchezo wa mapema utawakutanisha Namungo na TRA United kwenye Uwanja wa Majaliwa, mkoani Lindi kuanzia saa 10:00 alasiri, Namungo ikiingia kwenye mchezo huo ikiwa katika…

Cynthia Michael · Read more

MPANZU,FEISAL VIONGOZI MBIO ZA KUPIKA MABAO.

VITA ya pasi za mabao imezidi kushika kasi kutokana na namna wachezaji mbalimbali wanavyopambana kuhakikisha wanazidi kusaidia timu zao kupata alama za Ligi Kuu ya NBC. Kiungo Elie Mpanzu wa Simba ndio kinara wa kutoa pasi za mwisho amefanikiwa kucheza dakika 1187 ndani ya michezo 21 ya Ligi Kuu ya NBC akitoa pasi za mabao…

Loveness Bernard · Read more

LIGI KUU YA NBC HAKUNA ‘KUPOA’.

MZUNGUKO wa 27 wa Ligi Kuu ya NBC utaanza leo katika uwanja wa KMC Complex Dar es Salaam huku KMC na Coastal Union zikitarajia kufungua pazia la mzunguko huo saa 10:00 alasiri. KMC ambayo tayari imeaga Ligi Kuu ya NBC baada ya kupoteza mchezo uliopita dhidi ya TRA itakuwa na ‘kibarua’ cha kuwapa furaha mashabiki…

Loveness Bernard · Read more