News

Announcements, match reports and updates from the Tanzania Premier League Board.

RATIBA YA LIGI KUU YA NBC 2026/2027

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) leo Julai 20, 2026 imetangaza ratiba ya Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2026/2027. Bonyeza kiunganishi (Link) hapa chini kupakua ratiba hii. RATIBA YA LIGI KUU YA NBC 2026 /2027

Yahaya Abushehe · Read more

YOUNG AFRICANS ‘MBABE’ WA LIGI KUU YA NBC MSIMU WA 2025/26.

TIMU ya Young Africans wamehitimisha kwa mafanikio makubwa msimu wa Ligi Kuu ya NBC 2025/26 kwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya JKT Tanzania katika moja ya mchezo wa mwisho wa msimu uliochezwa Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo na kukabidhiwa rasmi taji la ubingwa. Prince Dube, Max Nzengeli na Laurindo Dilson ‘Depu’…

Cynthia Michael · Read more

PAZIA LA LIGI KUU YA NBC 2025/26 KUFUNGWA LEO.

Baada ya miezi kadhaa ya ushindani wa hali ya juu leo Juni 30, 2026, msimu wa Ligi Kuu ya NBC 2025/26 unafikia tamati rasmi kwa kuchezwa kwa michezo yote ya mwisho ya ligi. Mechi zote zitapigwa kwa wakati mmoja kuanzia saa 10:00 alasiri, hatua inayotarajiwa kuleta msisimko mkubwa kwa mashabiki wa soka nchini.…

Cynthia Michael · Read more

LIGI KUU YA NBC YAPAMBA MOTO LEO KWA MICHEZO NANE.

Ligi Kuu ya NBC msimu 2025/26 inaendelea leo Juni 27, kwa michezo nane itakayochezwa kwa wakati mmoja kuanzia saa 10:00 jioni. Timu mbalimbali zinashuka dimbani zikiwa na malengo tofauti, ikiwemo kusaka ubingwa, nafasi za juu, pamoja na kupambana kujinasua kwenye hatari ya kushuka daraja. Ratiba ya mechi za leo ni kama…

Cynthia Michael · Read more

MPANZU KINARA WA KUPIKA MABAO YA LIGI KUU YA NBC.

Kiungo mshambuliaji wa Simba, Elie Mpanzu, ameendelea kuthibitisha ubora wake katika Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2025/26 baada ya kuongoza orodha ya wachezaji wenye pasi nyingi za mabao kufikia sasa akiwa ametoa tisa (9). Mpanzu amekuwa mhimili muhimu katika safu ya ushambuliaji ya Simba , akichangia si tu kwa ubunifu wa kutengeneza nafasi…

Cynthia Michael · Read more

MOSSI, FEISAL HAPATOSHI VITA YA UFUNGAJI BORA

VITA ya ufungaji bora wa Ligi Kuu ya NBC imeanza upya baada ya mshambuliaji wa Singida Black Stars Mossi Ndumumwe kufikia idadi ya mabao aliyokuwa nayo kiungo wa Azam,Feisal Salum. Mossi Ndumumwe anaekipiga kunako Singida Black Stars amecheza michezo 20 sawa na dakika 1622 huku akifanikiwa kuingia nyavuni mara 14 pasipo kuwa na bao lolote…

Loveness Bernard · Read more

YOUNG AFRICANS,SIMBA ZATAMBA MZUNGUKO 28 LIGI KUU YA NBC.

MZUNGUKO wa 28 wa Ligi Kuu ya NBC umetamatika ambapo mechi zote nane zimechezwa majira ya saa kumi jioni huku ikisalia mizunguko miwili Ligi hiyo kutamatika. Young Africans ilikuwa mwenyeji wa timu ya Azam katika uwanja wa Amaan Zanzibar ambapo iliishushia kipigo cha mabao 3-0 yalifungwa na Ibrahim Hamad, Laurindo Dilson na Pacome Zouzoua hivyo…

Loveness Bernard · Read more

NANE ZA MOTO LIGI KUU YA NBC.

LIGI Kuu ya NBC itaendelea leo kwa michezo yote nane kupigwa saa 10:00 alasiri ikiwa mbashara katika chaneli mbalimbali za Azam Tv. Visiwani Zanzibar katika uwanja wa New Amaan itapigwa ‘Dabi’ ya Dar es Salaam kati ya Young Africans itakayokuwa mwenyeji wa Azam. Mchezo huo ndio mkubwa kwa leo ambapo wababe hao wapo katika mbio…

Loveness Bernard · Read more