News

Announcements, match reports and updates from the Tanzania Premier League Board.

KARIAKOO DABI KUPIGWA MEJA JENERALI ISAMUHYO.

BODI ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) inatangaza mabadiliko ya uwanja wa mchezo namba 169 wa Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2025/2026, kati ya klabu ya Simba na klabu ya Young Africans, maarufu kama ‘Kariakoo Derby’. Mchezo huo ambao hapo awali ulipangwa kufanyika kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa, sasa utachezwa kwenye uwanja wa Mej. Jenerali…

Loveness Bernard · Read more

BODI YA LIGI KUU TANZANIA (TPLB) KUPOKEA MABORESHO YA KANUNI ZA LIGI

BODI ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) inautaarifu umma kuwa imeanza kupokea maoni ya maboresho ya Kanuni za Ligi kwa toleo la mwaka 2026. Maoni/mapendekezo hayo ya maboresho ya kanuni ni kwa ajili ya Ligi Kuu Ligi ya Championship na First League. Lengo la zoezi hili ni kuboresha Kanuni za Ligi ili ziweze kutatua changamoto zilizojitokeza…

Loveness Bernard · Read more

CHIRWA KINARA WA MABAO NBC CHAMPIONSHIP.

LIGI ya Championship ya NBC msimu wa 2025/26 inaendelea kushika kasi huku vita ya ufungaji ikizidi kupamba moto huku wachezaji mbalimbali wakionyesha uwezo wao wa kutikisa nyavu. Kinara wa orodha hiyo anaekipiga katika kikosi cha Kagera sugar Obrey Chirwa tayari ameweka kambani mabao 14 na kuwa kileleni mwa wafungaji. Akifuatiwa na Adam…

Cynthia Michael · Read more

‘WANANCHI’ WATIKISA KWA VIPIGO VIZITO LIGI KUU YA NBC.

KWENYE msimu huu wa Ligi Kuu ya NBC klabu ya Young Africans imejijengea heshima kubwa si tu kwa kushinda michezo yake bali namna inavyoshinda kwa mabao mengi na soka la kuvutia linaloacha alama kwa mashabiki na wapinzani wao. Katika msimu huu, Young Africans imeonyesha ubora wa kipekee kwenye safu ya ushambuliaji kwa kutoa vipigo vizito kwa…

Honest Mwanitega · Read more

GEITA GOLD HAISHIKIKI, LIGI YA CHAMPIONSHIP YA NBC IKIPAMBA MOTO.

LIGI ya Championship ya NBC msimu wa 2025/26 imezidi kupamba moto huku ushindani ukiwa mkali katika kila kona ya msimamo, wakati mzunguko wa 22 ukielekea kufungwa rasmi. Vinara Geita Gold wameendelea kuthibitisha ubora wao baada ya kuichapa Hausung mabao 6-1 katika mchezo uliopigwa Uwanja wa Nyankumbu mkoani Geita huku ushindi huo wa kishindo ukiifanya Geita…

Yahaya Abushehe · Read more

SIMBA YAICHAPA NAMUNGO LIGI KUU YA NBC.

LIGI Kuu ya NBC imeendelea kwa mchezo mmoja ambapo Namungo walikuwa wenyeji wakiikaribisha Simba katika mchezo uliochezwa majira ya saa kumi jioni katika uwanja wa Majaliwa mkoani Lindi. Mchezo huo ulimalizika kwa Simba kupata ushidi wa mabao 3-1 huku wakionyesha ubora wao hasa katika kipindi cha kwanza walipofanikiwa kupata bao la mapema kupitia kwa Libasse…

Cynthia Michael · Read more

SIMBA, COASTAL ZAGAWA ‘DOZI’ LIGI KUU YA NBC.

LIGI Kuu ya NBC imeendelea kwa michezo iliyochezwa katika mikoa miwili tofauti ambapo Simba ilikuwa ugenini dhidi ya Fountain gate mchezo uliochezwa uwanja wa Sheikh Abeid mkoani Arusha na ‘Mnyama’ kusibuka na ushindi wa mabao 3-0. Simba walidhibiti mchezo kuanzia mwanzo hadi mwisho wakionyesha ubora mkubwa wa kushambulia na bao la kwanza lilifungwa mwishoni mwa…

Cynthia Michael · Read more