News

Announcements, match reports and updates from the Tanzania Premier League Board.

NBC CHAMPIONSHIP KUPIGWA MIKOA MITATU TOFAUTI LEO.

LIGI ya NBC Championship inaendelea leo Januari 6, 2024 kwa michezo minne kuchezwa kwenye mikoa mitatu tofauti. Michezo ya mapema saa 8:00 mchana itazikutanisha Pan African na Copco katika uwanja wa Mabatini mkoani Pwani, na mchezo mwingine Polisi Tanzania watawaalika Mbeya Kwanza katika uwanja wa Ushirika, Kilimanjaro. Green Warriors watakuwa wenyeji wa Mbeya City…

Yahaya Abushehe · Read more

NBC CHAMPIONSHIP KUREJEA LEO, TRANSIT CAMP KUWAVAA KEN GOLD.

Ligi ya NBC Championship inaendelea leo kwa Mchezo mmoja kati ya Transit Camp na Ken Gold saa 10:00 alasiri kwenye uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro. Transit Camp wapo nafasi ya 13 wakiwa na alama 13 baada ya michezo 15 huku Ken Gold wakiwa kileleni mwa msimamo wakiwa na alama 35 baada ya michezo 15.…

Yahaya Abushehe · Read more

SIMBA KUTAMATISHA HATUA YA MAKUNDI KOMBE LA MAPINDUZI LEO NA APR.

Mwakilishi wa Ligi Kuu ya NBC Simba anahitimisha hatua ya makundi ya kombe la Mapinduzi leo kwa mchezo dhidi ya wababe wa Rwanda APR saa 2:15 usiku kwenye uwanja wa New Amaan Complex. Simba inaingia katika mchezo huu akiwa kileleni mwa msimamo wa kundi B baada ya kushinda michezo yote miwili ya mwanzo dhidi…

Yahaya Abushehe · Read more

YANGA YAMALIZA HATUA YA MAKUNDI KOMBE LA MAPINDUZI NA SULUHU.

Mwakilishi wa Ligi Kuu ya NBC Yanga amemaliza michezo yake ya hatua ya makundi ya Kombe la Mapinduzi kwa suluhu dhidi ya KVZ. Yanga amemaliza kinara wa kundi C baada ya kushinda michezo miwili na kupata sare mchezo mmoja hivyo kufikisha jumla ya alama saba ambazo hakuna timu katika kundi hilo ambayo inaweza kufikia…

Yahaya Abushehe · Read more

YANGA KUIPEPERUSHA BENDERA YA LIGI KUU YA NBC KOMBE LA MAPINDUZI LEO.

KOMBE la Mapinduzi linaendelea leo huko Visiwani Zanzibar, saa 2:15 usiku wawakilishi wengine wa Ligi Kuu ya NBC Yanga watakukatana KVZ katika mchezo wa mwisho wa kundi C. Yanga wanaongoza kundi hilo wakiwa na alama sita baada ya michezo miwili huku KVZ wakiwa na alama nne baada ya michezo miwili. Jana mchezo wa wawakilishi…

Yahaya Abushehe · Read more

SIMBA, SINGIDA FG NI VITA YA LIGI KUU YA NBC NDANI YA MAPINDUZI CUP

KOMBE la Mapinduzi linaendelea leo visiwani Zanzibar kwa mchezo wa ‘miamba’ ya Ligi Kuu ya NBC kati ya Simba na Singida Fountain Gate saa 2:15 katika uwanja wa New Amaan Complex. Simba na Singida FG wapo Kundi B katika michuano hiyo ya Mapinduzi ambapo Simba ana alama 3 baada ya kucheza mchezo mmoja huku…

Yahaya Abushehe · Read more

KMC, TABORA UTD KUZIKABILI SIMBA NA YANGA LIGI KUU YA NBC LEO.

MCHAKAMCHAKA wa Ligi Kuu ya NBC unaendelea tena leo kwa michezo miwili ya ‘kibingwa’ kwenye mikoa miwili tofauti. Saa 10:00 alasiri KMC wataialika Simba katika uwanja wa Azam Complex mkoani Dar es salaam. KMC itatumia uwanja wa Azam Complex kama uwanja wao wa Nyumbani baada ya uwanja wa Uhuru kuwa katika marekebisho. Tabora United…

Yahaya Abushehe · Read more

AZAM HAIKAMATIKI, TANZANIA PRISONS, GEITA ZATAKATA LIGI KUU YA NBC.

LADHA ya Ligi Kuu ya NBC iliendelea leo kwa michezo mitatu iliyochezwa kwenye viwanja vitatu tofauti. Saa 8:00 mchana Tanzania Prisons walikua wenyeji wa Namungo katika uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya ambapo mchezo huo ulimalizika kwa Tanzania Prisons kuibuka na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Samson Mbangula dakika ya 42 ya mchezo. Saa 10:00…

Yahaya Abushehe · Read more

LIGI KUU YA NBC KUPIGWA MIKOA MITATU TOFAUTI LEO.

LIGI KUU ya NBC inaendelea leo kwa michezo mitatu katika mikoa mitatu tofauti baada ya kusimama kwa siku moja. Mchezo wa kwanza utazikutanisha Tanzania Prisons dhidi ya Namungo katika uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya saa 8:00 Mchana. Geita Gold watawaalika Singida FG katika uwanja wa Nyankumbu, Geita saa 10:00 alasiri. Mchezo wa mwisho utapigwa…

Yahaya Abushehe · Read more